Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo kushoto na akikabidhiwa Msaada wa Laptop 200 zenye thamani ya zaidi ya Shil.Millioni 400 kutoka kwa Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar Francesca Morandin ili kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara hiyo. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar
Francesca Morandin akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Msaada wa
Laptop 200 zenye thamani ya zaidi ya Shil.Millioni 400 kwa Wizara ya
Afya Zanzibar ili zisaidie kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za
Afya kwa wizara hiyo. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud
Thabit Kombo akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Msaada wa
Laptop 200 zenye thamani ya zaidi ya Shil.Millioni 400 kutoka shirika la
UNICEF ili kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara
hiyo.
Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
……………..
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Shirika la Umoja wa Mataifa la
kuhudumia Watoto UNICEF limetoa msaada wa Komputa aina ya Laptop 200 kwa
Wizara ya Afya ya Zanzibar ili kuimarisha usimamizi wa mfumo wa taarifa
za Afya kwa wizara hiyo.
Laptop hizo zenye thamani ya zaidi
ya Shilingi Milioni 400 zimetolewa ikiwa ni mwendelezo wa UNICEF
kuiunga mkono Serikali katika kuimarisha huduma za matibabu hasa ya
akinamama na watoto.
Akikabidhi Msaada huo katika
Ukumbi wa Wizara hiyo Mnazi mmoja Mwakilishi wa UNICEF Zanzibar
Francesca Morandin amesema upatikanaji wa taarifa sahihi ni jambo muhimu
linalofaa kupewa kipaumbele.
Amesema uwepo wa taarifa sahihi za
Wajawazito na watoto huisaidia Serikali kujua idadi ya ongezeko la watu
wake hali inayopelekea kupanga mipango vyema ya matibabu kulingana na
idadi ya watu husika.
Amewataka Watendaji kwa ujumla
kuunga mkono juhudi zinazotolewa na UNECO ili kuhakikisha afya za Watoto
na Wajawazito zinaimarika.
Francesca ameongeza kuwa Shirika
hilo la UNICEF litaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika juhudi zake za
kimatibu na kuipongeza Srikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea
kutoa matibabu bure kwa wananchi wake.
Amefahamisha kuwa Zanzibar inapiga
hatua mbele kwa upande wa Matibabu na kupongeza juhudi zinazofanywa na
Serikali kuwashajiisha Wajawajizito kushiriki huduma hizo muhimu katika
maisha yao. “Zanzibar zaidi ya asilimia 99 ya Wajawazito hushiriki
katika Kliniki mbalimbali walau mara moja katika kipindi chao cha
ujauzito. Hii inawezekana kwamba imechangiwa na juhudi za Serikali za
kuyafanya matibabu bure”Alipongeza Francesca.
Kwa upande wake Waziri wa Afya wa
Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amelishukuru Shirika la UNICEF kwa
kuendelea kuiunga mkono Zanzibar hasa katika sekta ya Afya.
Amemuahidi Mwakilishi huyo kwamba Msaada uliotolewa utatumika vyema ili kutimiza malengo ya Shirika hilo.
“Cha bure mara nyingi vitu vya
bure havitunzwi vyema lakini Laptop hizi lazima tujitahidi kuutumia
vyema..Laptop ziendelee kudumu na taarifa zinazohitajika zote kuanzia
Dawa, Wajawazito, Watoto nakadhalika zote ziwekwe kwenye mfumo
unaotakiwa”Alisema Waziri Kombo.
Waziri Kombo amesema Zanzibar
inaendelea kupokea pongezi kutoka pande zote za Dunia kwa namna Serikali
inavyojitahidi katika kutoa huduma bora za matibabu na hivyo msaada huo
utazidi kuimarisha huduma hizo.
Laptop hizo zitagawiwa katika
Vituo vyote vya matibabu Unguja na Pemba ili kuimarisha usimamizi wa
mfumo wa taarifa za Afya kwa wizara hiyo.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR