Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akionesha
Mwongozo wa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano mara baada ya
kukabidhiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kwa
niaba ya Wabunge. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Spika,
Bungeni mjini Dodoma Februari 8, 2018.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto)
akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia
Ackson (wa pili kulia) Mwongozo wa
watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kwa niaba ya Wabunge.
Wakishuhudia watatu kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu wa Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete na wa pili kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba. Makabidhiano hayo yamefanyika
ofisini kwa Naibu Spika, Bungeni mjini Dodoma Februari 8, 2018.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto)
akimweleza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia
Ackson (wa kwanza kulia) umuhimu wa
Mwongozo wa watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kwa Wabunge mara baada
ya kumkabidhi Mwongozo huo kwa niaba ya Wabunge ili waweze kusoma, kuelewa na
kuelimisha wananchi namna ya kutumia vema huduma na bidhaa za mawasiliano
nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Spika, Bungeni mjini
Dodoma.
Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson (wa kwanza kulia) kuhusu Mwongozo wa
watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano mara baada ya kukabidhiwa na Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kwa niaba ya Wabunge. Makabidhiano
hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Spika, Bungeni mjini Dodoma