Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza waliovamia
eneo la Mkesa ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU
iliyopo Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara na Naibu Waziri wa
Tamisemi, Joseph kakunda kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza
wananchi hao kwa ajili ya kujionea uharibifu unaoendelea katika eneo
hilo . Wengine ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili
kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo (katikati
Naibu
Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (katikati) akizungumza na Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( kulia) pamoja na na Mkuu
wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo (kushoto) ofisis kwa mkuu wa wilaya
hiyo kabla ya kuanza kwa ziara iliyofanyika jana ya kutembelea eneo la
Mkesa liliopo ndani ya Jumuiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU kwa
lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea
katika eneo hilo.
Naibu
Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda akizungumza na wananchi waliovamia
eneo la Mkesa ndani ya Jumiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo
Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara na Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii, Japhet Hasunga kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza
wananchi hao kwa ajili ya kujionea uharibifu unaoendelea katika eneo
hilo . Wengine ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili
kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo (katikatiNaibu
Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia) Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) pamoja na na Mkuu
wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo ( wa pili kushoto) wakiangalia
nyaraka feki iliyowasilishwa na miongoni mwa wananachi aliyedai kuwa
yeye ni mkazi halali katiaka eneo hilo la Mkesa liliopo ndani ya Jumuiya
Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU wakatia wa ziara iliyofanyika jana
ikiwa na Manaibu wa wawili wa Maliasili na Utalii pamoja na wa TAMISEMI.Mkuu
wa wilaya ya Morogoro akizungumza na wananchi waliovamia eneo la Mkesa
lililopo ndani ya Jumuiya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo
Morogoro vijijini wakati walipofanya ziara akiwa ameongozana na Manaibu
wawili wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga pamoja na Naibu
Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda wakati walipotembelea eneo hilo kwa
lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea
katika .
Naibu
Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda (wa pili kulia akiwa na Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ( wa kwanza kulia) pamoja na na
Mkuu wa wilaya ya Morogoro,Regina Chonjo ( wa pili kushoto)
wakimsikiliza miongoni mwa wananachi aliyedai kuwa yeye ni mkazi halali
katika eneo hilo la Mkesa liliopo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya JUKUMU wakati wa ziara iliyofanyika jana kwa ajili ya
kuwasikiliza wananchi hao na kujionea uharibifu unaoendelea katika .Baadhi
wananchi wakiwasilikiliza Manaibu Waziri katika mkutano uliofanyiak
jana katika eneo la Mkesa lililopo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya
Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo Morogoro vijijini wakati wakati wa ziara
kutembelea eneo hilo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kujionea
uharibifu unaoendelea katika .Naye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya JUKUMU, Shaban
Kolahili akisalimia na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet
Hasunga wakati Naibu Waziri huyo alipowasili katika kijiji cha Mbwade
akiwa ameongozana naNaibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda.
( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA- MNRT
Serikali
kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na wa TAMISEMI imetoa siku
saba kwa wananchi waliovamia kwa kuendesha maisha yao na kufanya
shughuli za kilimo pamoja na kulisha mifugo ndani ya Jumuiya ya Hifadhi
ya Wanyamapori ya JUKUMU iliyopo katika Halmashuri ya Morogoro vijijini
kuondoka katika hifadhi hiyo.
Hali
hiyo inafuatia baada ya wananchi hao kwenda mjini Dodoma kuonana na
Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa na kumuelezea malalamiko yao kuwa wao ni
wakazi halali katika eneo hilo lakini hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya hiyo,
Regina Chonjo amekuwa akiwalazimisha kuondoka.
Kufuatia
hali hiyo , Waziri Mkuu K Majaliwa alimuagiza Waziri wa Maliasili na
Utalii pamoja na Waziri wa TAMISEMI kwenda huko kwa ajili ya
kushughulikia tatizo hilo ambapo Mawaziri hao kutokana na kubwana na
majukumu mengine waliwaagiza Manaibu Waziri wao kutembelea eneo. .
Katika
ziara hiyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga pamoja
na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Joseph Kakunda jana walitembelea eneo hilo
na kujionea uharibifu unaoendelea.Katika ziarz hiyo Manaibu Waziri hao
walizungumza na wananchi hao kwa kumtaka mwananchi yeyote mwenye nyaraka
halali za kuishi katika eneo hilo aziwasilishe katika mkutano huo
lakini hata hivyo hakuna mwananchi yeyote aliyeziwasilisha
Kutokana
na wananchi hao kukiri kuishi kinyume na sheria katika eneo hilo la
Hifadhi, Wananchi hao waliowaomba viongozi hao wapewe muda ili waweze
kutafuta sehemu ya kuhamia kwa vile hawana sehemu ya kwenda,Kulingana
uharibifu mkubwa waliojionea katika eneo hilo hali ya mazingira, Mnaaibu
Waziri hao waliweza kuagiza mambo yafuatayo huyo. Kama.
Manaibu
Waziri hao waliagiza kuwa materekta yote yatakayoonekana katika eneo
hilo la hifadhi baada ya siku saba kupita yataifishwe.Pia, Waliagiza
kuwa yakamatwe na hatimaye kupigwa mnada kwa mujibu wa sheria kwa mifugo
yote itakayooneka katika eneo hilo la hifadhi.Aidha, Waliagiza kuwa
mwananchi yeyote atakayekutwa ndani ya hifadhi hiyo baada ya siku saba
kuwa atakamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kuvamia hifadhi.
Awali,
Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo aliwaeleza Manaibu Waziri hao kuwa
wananchi hao wamekuwa wakilima na kuchunga mifugo katika maeneo hayo
hali iliyopelekea wanyamapori katika maeneo hayo kuhama.Naye Mwenyekiti
wa Jumuiya ya JUKUMU, Shaban Kolahili ameiomba Wizara ya Maliasili na
Utalii iwasaidie kuhakikisha kuwa hifadhi hhiyo inalindwa ili kuzuia
vitendo vya ujangili na uvamizi unaoendelea ili kuwavutia wawekezaji ili
hatimaye iweze kujitegemea.
Wananchi
wa eneo hilo mnamo mwaka 2010 walituma maombi kwa Wizara ya Maliasili
na Utalii ya kuomba wasaidiwe katika kulihifadhi eneo hilo ambalo
hutumiwa na wanyapori kupimzika na kuzaliana