Bibi Fatuma Kimario, Meneja
Msaidizi Idara ya Kudhamini Mikopo, Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
akitoa mada juu ya Mfuko huo unavyofanya kazi kwenye semina ya
waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha inayofanyika mkoani
Mtwara Februari 5, 2018.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KIASI cha Shilingi trilioni 1.30 kimetolewa kama dhamana
ya mkopo chini ya uchamini wa Mfuko wa Udhamini wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT)
kwa taasisi 87 zinazojishughulisha na kuuza mazao nje ya nchi, (ECGS) na Sekta
ya Wajasiriamali wadogo na wakati (SME-CGS), Meneja Msaidizi Idara ya Kudhamini
Mikopo ya benki hiyo Bibi. Fatma Kimario amesema.
Akiwasilisha mada kwenye semina ya waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na
Fedha, inayoendelea mjini Mtwara, Februari 5, 2018 Bibi Kimario alisema,
kupitia Mfuko wa Udhamini wa Mauzo nje
ya Nchi (ECGS), na Sekta ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati, (SME-CGS) udhamini
huo ni wa mkopo wa fedha wa kiasi cha shilingi trilioni 1.70 zilizotolewa na
taasisi za fedha ili kukopesha wanufaika
hao.
Akifafanua zaidi Bibi Kimario alisema, “Sekta
zilizonufaika chini ya Mfuko wa kudhamini Mauzo nje ya nchi (ECGS) ni 21 ambapo
taasisi za fedha zilitoa mikopo kwa sekta 21 ambazo ni pamoja na
Kilimo, Viwanda,
Uchimbaji na Uvuvi ambazo kwa ujumla wake zilipata mikopo ya jumla ya shilingi
trilioni 1.65, ambapo Mfuko wa Udhamini ulitumia kiasi cha shilingi trilioni
1.25 kudhamini mkopo huo” Alifafanua.
Akifafanua zaidi, Mtaalamu huyo kutoka BoT, alisema,
sekta ya Kilimo ndiyo iliyonufaika zaidi kwa kupata mkopo wa shilingi trilioni
1.52, Viwanda bilioni 101, Uchimbaji, shilingi bilioni 14 na Uvuvi bilioni 4.5 .
Kwa upande wa Sekta ya Wajasiriamali Wadogo na wa
Kati, (SME-CGS), taasisi 65 zilinufaika kwa kupata mkopo wa jumla ya
shilingi bilioni
10.52 ambapo Mfuko ulitumia kiasi cha shilingi bilioni 5.14 kudhamini mkopo
huo.
Akifafanua jinsi sekta hizo zilivyonufaika Bibi
Kimario alisema “Sekta ya Kilimo ndiyo iliyoongoza kwa kupata mkopo wa shilingi
bilioni 4.8, Viwanda bilioni 1.5, Ujenzi bilioni 1.4, Elimu milioni 930, Utalii
milioni 874, Mawasiliono milioni 570, Huduma 130, Uchimbaji madini milioni 68,
Afya milioni 63, Uvuvi milioni 50, na Uchukuzi milioni 34.”
Alisema.
Bibi Kimario ameelezea utaratibu wa udhamini umekuwa
wa mafanikio makubwa ambapo kwa kuongezeka kwa pato la Halmashauri ambazo vyama
vya Ushirika vya Msingi vilivyodhaminiwa na mfuko huu.
Kuchangia ongezeko la fedha za kigeni kutokana na
mauzo ya nje ya nchi kuchangia makusanyo ya kodi kwa serikali zitokanazo na bidhaa za
viwandani.
Dkt.Suleiman Missango, Meneja
Msaidizi Idara ya Utafiti Kurugenzi ya Sera za Uchumi na Utafiti BoT,
akifafanua baadhi ya mambo yahusuyo utekelezaji wa majukumbu
mbalimbali ya BoT.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia
semina hiyo.
Baadhi ya washiriki
wakifuatilia semina hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha
Uhusiano na Itifaki cha BoT, Bibi. Zalia Mbeo, (mbele) akiwa na
wataalamu wa benki hiyo wakati wa semina hiyo.
Bibi. Grace
Aswile, Meneja Msaidizi-Idara ya Masoko ya Ndani ya Fedha kutoka Benki
Kuu ya Tanzania, (BoT), akiwasilisha mada kuhusu utaratibu wa
kuendesha soko la dhamana za serikali ambapo pamoja na mambo mengine
alisema, BoT inaendelea na uhamasishaji
na elimu kwa umma
wa watanzania wote kushiriki
katika minada hii kama
njia moja wapo ya
kujiwekea akiba na kuchangia
shughuli za uchumi wa nchi
yetu.
Bibi. Grace Aswile, Meneja Msaidizi-Idara ya Masoko ya Ndani
ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), akiwasilisha mada kuhusu
utaratibu wa kuendesha soko la dhamana za serikali
Meneja Usimamizi wa
Mabenki wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Eliamringi
Mandari, akitoa mada kuhusu Kanuni mpya za maduka ya kubadilisha fedha
yaani (Bureaux de change). chini ya kanuni hii wamiliki wanatakiwa
kuonyesha viwango vya kubadilisha fedha sehemu ya uwazi na waonyeshe
leseni ya BoT ikiwa ni pamoja na kutoa Fiscal receipt(EFDs) kwa wateja
wao.
Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusoano wa Umma na Itifaki, Benki
Kuu ya Tanzania, (BoT), Bi. Vicky Msina, (kushoto) akiwa na Bw.Sadiki
Nyanzowa, ambaye ni Afisa Msaidizi-Idara ya Udhamini wa Mikopo
BoT.
Afisa Uhusiano
Mkuu kutoka Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bw. Lwaga
Mwambande