Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS), Bw. Hija Malamla akizungumza katika kikao cha
pamoja kati ya wataalamu wa sekta ya barabara nchini na ujumbe wa Waziri wa
Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Lesotho uliko nchini kwa ziara ya mafunzo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART),
Eng. Ronald Lwakatare (aliyesimama) akifafanua jambo kwa ujumbe wa Waziri wa
Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Lesotho walipotembelea mradi huo.
Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi cha Wakala wa Barabara
nchini (TANROADS), Bw. Lyanga (wa pili kushoto) akiwasilisha mada kwa ujumbe wa
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Lesotho walipotembelea ofisi za TANROADS
jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa
Lesotho, Mathabathe Hlalele (wa pili kulia) akisisitiza jambo kwenye kikao cha
kubadilishana uzoefu kati ya ujumbe wa nchi hiyo na Tanzania.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Lehlohonolo
Moramotse (wa tatu kulia) akisisitiza jambo akiwa kwenye moja ya Mabasi
yaendayo haraka (DART) alipotembelea mradi huo jijini Dar es Salaam. Wa pili
kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART), Eng. Ronald
Lwakatare.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mabasi yaendayo haraka (DART),
Eng. Ronald Lwakatare (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi wa Lesotho, Mhe. Moramotse (kulia) alipo tembelea kukagua mradi huo.
Imetolewa
na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.