Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi
kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani. Wa Pili kushoto anayevuta
utepe ni Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu ya
Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian na wa kwanza kushoto anayepiga
makofi ni Balozi wa China hapa nchini Wang Ke
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (CDF)
Jenerali Venance Mabeyo mara baada ya kufungua Kituo hicho cha Mafunzo
Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimshukuru Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu
ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara baada ya ufunguzi wa
kituo hicho ambacho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la
watu wa China.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Husein
Mwinyi wakati alipokuwa akiandika jambo katika hotuba yake.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akihutubia wananchi mara baada ya kufungua Kituo cha Mafunzo Maalum ya
Kijeshi kilichopo Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke mara baada ya
kukifungua kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Naibu Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mafunzo kutoka tume Kuu
ya Kijeshi ya China Meja Jenerali Yang Jian mara baada ya kukifungua
kituo hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Mbunge wa Bagamoyo Dkt.
Shukuru Kawambwa, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete pamoja na Mkuu wa
mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kufungua kituo
hicho cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na wananchi wa Mapinga(hawaonekani pichani) waliokuwa
wakiwasilisha kero mbalimbali za ardhi wakati alipokuwa akirejea jijini
jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua kituo hicho cha Mafunzo
Maalum ya Kijeshi kilichopo Mapinga mkoani Pwani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na Makomandoo wa JWTZ ambao walishiriki
katika mazoezi ya Kijeshi kabla ya ufunguzi wa kituo hicho.
Kikundi cha Ngoma za asili cha
Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikitumbuiza wakati wa
sherehe za ufunguzi wa kituo hicho cha Mafunzo maalum ya Kijeshi
kilichopo Mapinga mkoani Pwani. PICHA NA IKULU