Mmoja wa akina mama wa kijiji cha
Mauno, Kata ya Bumbuta, Jimbo la Kondoa Vijijini akiongea na vyombo vya
habari kuhusu furaha yao baada ya kisima cha maji kuzinduliwa hatua
iliyowaondolea kero ya kutembea mwendo mrefu kutafuta maji
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,
na Mbunge wa Jimbo la KOndoa Vijijini, Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafadhili wa mradi wa kisima
cha maji pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji na viongozi
wa dini katika kijiji cha Mauno, wilayani Kondoa.
Wanakijiji wa Kijiji cha Mauno
Wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakichota maji baada ya kuzinduliwa rasmi
kwa kisima cha maji kilichojengwa na wafadhili kutoka nchini Uturuki
kupitia Ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini.
Wanakijiji wa Kijiji cha Mauno
Wilayani Kondoa mkoani Dodoma wakichota maji baada ya kuzinduliwa rasmi
kwa kisima cha maji kilichojengwa na wafadhili kutoka nchini Uturuki
kupitia Ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini.
Wakazi wa kijiji cha Mauno
wakiwa wamemwangusha ng’ombe kwa ajili ya kupata kitoweo ikiwa ni namna
ya kujipongeza na kusherehekea baada ya kuzinduliwa kwa kisima cha maji
kilichojengwa na wafadhili kutoka nchini Uturuki.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango
……………………
Na Benny Mwaipaja, Kondoa
ZAIDI ya wakazi elfu 16 wa vijiji vitatu vya Mauno, Makiranya
na Kinyasi-Majengo, katika Jimbo la Kondoa Vijijini mkoani Dodoma
wameondokana na adha ya kukosa maji baada ya kuzinduliwa kwa visima
viatu vya maji vilivyojengwa kwa msaada wa wahisani kutoka nchini
Uturuki kupitia ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini
“Hivi sasa ujenzi wa visima 15 kati ya 25 vinavyojengwa na
Serikali kupitia Wizara ya Maji unaendelea huku wahisani wakiwa
wametujengea visima 36 hivyo kufikisha idadi ya visima 61 katika kipindi
cha miaka miwili tu tangu Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais Dkt.
John Pombe Magufuli aingie madarakani hali ambayo haijawahi kutokea na
lengo letu ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote 84 vinapatiwa huduma ya maji
ifikapo mwaka 2020” Alisisitiza Dkt. Kijaji
Diwani wa Kata ya Bunbuta Bw. Bashiru Mtolo na mkazi mmoja wa
kijiji hicho Bi. Khadija Hussein wamesema kuwa tatizo la maji katika
kijiji cha Mauno lilikuwa kubwa na kuwalazimisha wanawake na watoto
kwenda umbali mrefu kusaka maji kwa ajili ya matumizi yao ya majumbani
pamoja na kunywesha mifugo.
“Tunaushukuru Ubalozi wa Uturuki
kwa msaada wao huu mkubwa na Mbunge wetu kwa ufuatiliaji wake wa karibu
uliowezesha kupatikana kwa visima hivi na vingine ambavyo vimesaidia
kwa kiwango kikubwa kutatua kero ya maji na tunaamini mpaka kufikia
mwaka 2020, matatizo ya maji katika wilaya yetu ya Kondoa litakuwa
historia” alisema Diwani Mtolo.
Naye Mwakilishi na Mwambata wa
Ubalozi wa Uturuki hapa nchini Sheikh Muhammad Cicek ameeleza kuwa
msaada wa Dola elfu 36 zilizotumika kujenga miradi hiyo mitatu ya visima
vya maji umetolewa na wahisani mbalimbali wa Uturuki ikiwa ni kuenzi
uhusiano wa muda mrefu kati ya Uturuki na Tanzania.
Alisema kukamilika kwa miradi
hiyo ya maji kutasadia kuwawezesha akina mama na wananchi wa Kondoa kwa
ujumla kufanya shughuli nyingine za maendeleo badala ya kutumia muda
mwingi kutafuta maji ambayo hata hivyo hayakuwa safi wala salama.