Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo
akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika
Mkoa wa
Katavi ikiwa ni sehemu ya timu ya wataalamu 15 ya Wizara hiyo walioko
katika mikoa 26 ya Tanzania bara kufuatilia na kusimamia kikamilifu
zoezi la upigaji chapa ambapo Dk Mashingo alisema mifugo itakayokuwa
haijapigwa chapa hadi kufikia Januari 31 mwaka huu haijulikani Serikali
nini kuhusu mifugo hiyo.
NA MWANAHAMISI MSANGI, WMVU
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imeunda timu ya wataalamu 15 iliyopo katika
mikoa 26 ya Tanzania bara ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Mifugo) Dk.
Maria Mashingo kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa
mifugo yote nchini kabla ya kufika tarehe ya mwisho ya muda wa nyongeza wa Januari
31 mwaka huu.
Timu hiyo ya wataalamu imeanza kutekeleza majukumu yake Januari 4 mwaka
huu ambapo kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Maria Mashingo wilaya 30
ambazo bado hazijaanza zoezi la chapa na zimetiliwa mkazo katika ufuatiliaji ikiwemo
Monduli, Kilwa, Liwale, Ruangwa, Mafia.
Aidha, Wilaya nyingine ni Sikonge, Tabora, Urambo, Mwanza, Ilemela
Manispaa, Magu, Ukerewe, Buchosa, Tarime, Kyerwa, Ngara, Newala, Newala Mjini, Tandahimba,
Nanyamba, Mtwara, Mikindani Manispaa, Masasi, Masasi Mjini, Nanyumbu, Moshi DC,
Hai, Same, Rombo, na Kigamboni.
Dk. Mashingo amesema suala la
upigaji chapa mifugo lipo kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa mifugo Namba
12 ya Mwaka 2010 ili kudhibiti magonjwa
ya mifugo pamoja na wizi wa mifugo, kuimarisha
usalama wa afya na mazao ya mifugo pamoja na kudhibiti usafirishaji na uhamaji
holela wa mifugo.
Amesema jumla ya ng’ombe millioni 19, 219,487 sawa na theluthi mbili ya
ng’ombe wote milioni 28, 829,231 walioko
nchini ambapo mpaka sasa jumla ya ng’ombe milioni 7, 701,661 sawa na asilimia
38.5 ndio wamepigwa chapa ambapo wamechangia kiasi cha shs. Bilioni 3, 700,830,500
kwa malipo ya Tsh 500 kwa kila ng’ombe.
Hivyo, Tathmini iliyofanyika kutokana na taarifa zilizokusanywa kutoka
halmashauri zinaonesha kwamba, kati ya malengo waliojiwekea, Halmashauri 62
wamepiga chapa zaidi ya asilimia 50; Halmashauri 43 zimepiga kati ya asilimia
10 hadi 50; Halmashauri 23 zimepiga chini ya asilimia 10 na Halmashauri 30
hazijaanza lakini ziko kwenye maandalizi.
Ametaja baadhi ya changamoto zilizochangia kuathiri utekelezaji wa
zoezi la chapa ni wafugaji kukataliwa kupiga chapa mifugo yao kwa kisingizio
kuwa ni wavamizi na wahamiaji haramu katika Wilaya za Kibiti, Rufiji,
Sumbawanga, Tanganyika, Kibondo.
Pia kutofautiana kwa gharama za uchangiaji ambapo baadhi ya wafugaji
waliogomea kiwango cha sh 1000/= ambacho ni kinyume na kiwango elekezi cha sh
500/= kwa kila ng’ombe mfano katika Wilaya za Chunya na Tanganyika.
Vilevile fedha zilizochangwa kugharamia zoezi la chapa kutotolewa kwa
wakati katika baadhi ya Halmshauri ikiwemo Mbarali na Misungwi hivyo kukwamisha
utekelezaji wa kazi hiyo.
Timu hiyo ya watalaamu imegawanyika katika makundi saba kwenye mikoa ya
Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Singida, Dodoma, Morogoro, Pwani, Dar es
Salaam.
Mikoa mingine ni Tabora, Katavi,Rukwa, Kigoma, Shinyanga, Simiyu,
Mara,Mwanza, Geita, Kagera, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Ruvuma, Lindi na
Mtwara.