MBUNGE WA LUSHOTO KUWALIPA KADI ZA MATIBABU ZA (CHF) WAZEE WASIOJIWEZA KATA YA MLOLA

January 08, 2018
 Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi “Bosnia” akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani Lushoto mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara na kusikiliza kero zinazowakabili wakati wa ziara yake
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi “Bosnia” kulia akisikiliza kwa umakini maswali ya wananchi wa Kijiji cha Lwandai
Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi “Bosnia” akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho wakati wa ziara yake kusikiliza changamoto zinazowakabili
Mmoja wa wakazi wa Kijiji hicho akiuliza swali katika mkutano huo wa hadhara
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi “Bosnia” kushoto akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa CCM kata ya Mlola baada ya kumaliza mkutano wake na wananchi
  Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi “Bosnia” katikati akimsikiliza mkazi wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani Lushoto mara baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara.
MBUNGE wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia amesema atawalipia kadi za Afya ya Jamii (CHF) wazee wote wasiojiweza wenye umri wa miaka sitini na kuendelea waliopo kwenye kata ya Mlola wilayani Lushoto ili waweze kupata huduma za matibabu bure wakati wanapokuwa wakiugua.

Hatua ya mbunge huyo ina lengo la kusaidia matibabu kwa wazee hao kwani baadhi yao wanayakosa kutokana na kukosa fedha hiyo kupitia mpango huo wanaweza kutibiwa wakati wowote na kuondokana na changamoto zinazowakabili.

Aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani humo ambapo alisema wazee wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo hivyo wanapokosa huduma za matibabu kutokana na ukata wa fedha sio jambo nzuri kwani wanapaswa kusaidiwa.

“Kwa kweli kama mnavyojua ndugu zangu wazee wetu wana mchango mkubwa sana katika maendeleo lakini changamoto kubwa ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo kila wakati ni kuhusu gharama za matibabu wanapokuwa wakiugua hivyo mimi Mbunge wenu nimeona niwalipie “Alisema.

“Lakini pia nikuagize Afisa Mtendaji wa Kata ya Mlola, Saidi Kimweri uniorodheshehe majina ya wazee wote waliopo kwenye eneo lako ambao hawajiwezi kuanzia miaka sitini kwa lengo la kuweza kuwakatia kadi za CHF waweze kupata matibabu bure pia hakikisha unapita nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuwabaini wahusika “Alisema Mbunge huyo

Ahadi hiyo inatokana na swali lililoulizwa mkazi wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola Ayoub Fundi  kwa mbunge huyo katika mkutano wa hadhara kuhusu wazee wasiojiweza watasaidiwa vipi kuweza kupata huduma za matibabu katika vituo vya afya, zahanati na hospitali kutokana na uwezo mdogo walionao.

“Mh mbunge sisi wazee tusijiweza utatusaidiaje tuweze kupata matibabu tunapokuwa tukiugua maana tunakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa ni hasa namna ya kupata fedha zitakazo tusaidia kutibiwa wakati wa maradhi “Alisema.

Alisema kwani baadhi yao wamekuwa ni wazee sana na hivyo hawana namna ya kuweza kutafuta fedha za kuweza kusaidia kutibiwa wakati wanapokuwa wakiugua hivyo wanamuomba awasaidie kwenye jambo hilo ambalo ni muhimu kwa ustawi wa
maisha yao.

Kwa upande wake,Afisa Mtendaji huyo wa kata ya Mlola Saidi Kimweri alihaidi kutekeleza agizo hilo kwa vitendo na baadae kuweza kumfikishia ili aweze kusaidia jambo hilo ambalo litakuwa mkombozi mkubwa kwa wazee hao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »