BANDARI YA TANGA YAPOKEA BOTI YA DORIA

April 11, 2018


MENEJA wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimisho ya miaka 13 ya Mamlaka hiyo juzi kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
MENEJA wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

MENEJA wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akifuatilia matukio kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na kulia ni
MENEJA wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim
sehemu ya watumishi wa Bandari wakifuatilia matukio

Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto akipata maekelezo anayefuatia kushoto ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama

MENEJA wa Bandari ya Tanga Percival Salama kulia akimkabidhi zawadi mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa


BANDARI ya Tanga imepokea boti ya doria yenye thamani ya fedha za kimarekani UDS 2,204,100 kwa ajili ya kufanyia doria kwenye ukanda wa bahari

Boti hiyo ambayo imenunuliwa na mamlaka hiyo itakuwa na msaada mkubwa pia kukabiliana na wimbi la biashara haramu za magendo zinazoendelea kufanyika kwa zaidi ya bandari bubu 40 katika ukanda wa pwani mkoani hapa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Bandari Mkoani Tanga Percival Salama kwenye maadhimisho ya wiki ya Mamlaka hiyo Nchini Tanzania(TPA)Mkoani hapa kwa kufikisha miaka 13.

Aidha alisema boti hiyo yenye uwezo mkubwa itakuwa muarubaini kwa ajili ya kukabiliana na wafanya biashara za magendo katika bandari zisizo rasimishwa(bubu) ambapo itakuwa na kazi ya kufanya doria kukabiliana na wimbi hilo la magendo.

“Kweli biashara za magendo zimekithiri hasa katika ukanda wetu wa bahari ya hindi na sasa tayari tumepata boti mpya na ya kisasa kwa ya doria jukumu letu ni kukabiliana na wafanyabiashara hao tu na sivinginevyo”Alisema.

Salama alisema zipo bandari nyingi mkoani hapa ambazo sio rasmi na zinatumiwa na wafanyabiashara ambao si waaminifu kwa Serikali yao jambo ambalo limewalazimu mamalaka husika kutafuta chombokitakachokuwa na uwezo wa kufanya doria nyakati zote.

Alisema mkoani Tanga kuna Bandari mbili ambazo ni Tanga mjini na Pangani ndio ambazo zilizorasimishwa kihalali na mamlaka hiyo kwa ajili ya kufanya shughuli za usafirishajiwa mizigo mbali na zile za kipumbwi,mkwaja,kigombe jasini na nyinginezo ambazo hazitambuliwi kwa mujibu wa sheria.

Awali akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya Tanga Thobias Mwilapwa ambae alikuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo alisema serikali haitakuwa na mjadala na watu wanaojishughulisha na biashara hizo.

Aidha alisema kumekuwepo na wimbi la biashara hizo za magendo katika Bandari bubu ambapo kupitia kamati za ulinzi majeshi yote yataungana kwa ushirikiano na Mamlaka ya bandari kupambana na wafanya baishara hao.

“Labda niseme tu kinachofanyika tanga kama mazoea na sasa vita yakuwakabili wafanyabiashara hao itakuwa kubwa zaidi kama unayosikia kwawenzetu wa Bandari wameleta boti ya kisasa ya doria sisi tutaongeza nguvu ya kijeshi lazma tukomeshe biashara hizo”Alisema Mwilapwa.

Hata hivyo aliwasihi wafanyabiashara kuacha mara moja biashara hiyo ya magendo kutokana na Serikali kutoa maelekezo ya kutaifisha vyombo vitavyo kamatwa na bidhaa zote zitashikiliwa na serikali.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »