Katika Picha, Ng’ombe aina ya
Borani inayomilikwa na mwekezaji kampuni ya Overland katika Ranchi ya
Mzeri , Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Katikati Waziri wa Mifugo na
Uvuvi. Mhe. Luhaga Mpina akiongea vyombo vya habari baada ya ziara ya
ukaguzi wa baadhi ya vitalu katika Ranchi ya Mzeri iyopo Wilayani
Handeni Mkoani Tanga, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin
Gondwe, na kulia ni mkurugenzi wa kampuni ya Overland Bw. Faizal Edha.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina kati kati na Mkuu wa Wilaya ya Handeni kulia Godwin Gondwe pamoja
na wataalam kutoka Wizarani na Mkoani Tanga wakiwa katika zoezi la
kukagua baadhi ya vitalu vilivyopo katika Ranchi ya Mzeri Wilayani
Handeni.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina akikimkimbiza Ng’ombe aina ya Borani katika Ranchi ya Mzeri
alipokuwa katika zoezi la ukaguzi wa vitalu .
Aliyesimama Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akongea na Uongozi wa Wilaya ya Handeni na
wajumbe wa Msafara kabla ya kuanza kwa ziara katika Ranchi ya Mzeri kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe
……………
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.
Luhaga Mpina ameagiza kuvunjwa kwa mkataba ulioundwa baina ya RANCHI ya
Taifa NARCO na kampuni ya Overland kwa pamoja na kuunda kampuni ya
OVENCO uliyokuwa na mapungufu ya kisheria na kiutendaji kufunjwa ifikapo
mwisho wa mwezi huu wa December na kutoa mwezi mmoja kwa NARCO kuunda
mkataba mpya wenye mwengozo wa kisheria.
Mpina aliyasema hayo jana
alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa Ranchi ya Mzeri iliyopo wilayani
Handeni Mkoani Tanga yenye ukubwa kwa Hekta 41,000 ambapo hekta 21,000
zinamililiwa na Muwekezaji kampuni ya Overland muwekezaji ambaye,
amekuwa na mgogoro wa muda mrefu na NARCO ambapo baada ya Waziri Mpina
kusililiza pande zote mbili na kujiridhisha na kumuona muwekezaji
kutokuwa na uwezo wa kufikia malengo ya kuendeleza eneo lote la ardhi
ambalo amekuwa akiliendeleza bila makubaliano yoyote ya kisheria, jambo
ambalo limempelekea Waziri Mpina kuagiza NARCO kuingia katika hatua
ya kuunda mkataba mpya baina yake na muwekezaji huyo utakaozingatia
masharti mapya ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa muwakilishi wa
NARCO Katika kitalu hicho.
Aidha Waziri Mpina ameagiza
muwekezaji huyo asihamishwe kwa kuwa ameonyesha nia ya kuendeleza eneo
hilo kwa kuwepo kwa ng’ombe wambegu aina ya Borani pamoja na miundombinu
mingine
Akizungumzia eneo la hekta 20,000
linalomilikiwa na wawekezaji wengine wadogo, Mpina aliwataka wawekezaji
hao kulipa na kumaliza madeni yote ya kodi ya serikali wanayodaiwa
katika vitalu vyao ifikapo January mosi 2018.
“Wawekezaji wengine wengine
wanaomiliki vitalu katika ranchi hii ya Mzeri mnatakiwa kulipa madeni
yote ya kodi mnayodaiwa na Serikali kodi mnayolipa ya shilingi elfu moja
(1000) kwa mwaka ni kidogo sana lakini bado hamlipi, kinyume na hili ni
bora muondoke wenyewe au tutawaondosha kwa nguvu muda huo ukifika. “
Alisisitiza Mpina.
“Baada ya kumaliza kulipa nawagiza
NARCO kuwapa miezi mitatu wawekezaji hawa kuhakikisha wanaweka
miondombinu inayolingana na ukubwa wa eneo na matumizi ya ardhi ,
tunataka wawekezaji wafikie malengo na mashamba haya yafanye kazi.”
Alisema Mpina.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Handeni Godwin Gondwe alisema kuwa, Wiaya ya handeni itaendelea kulinda
mazao na rasilimali za Mifugo kupitia sheria ndogondogo ambazo wilaya
hiyo imejiwekea.
Akizungumza kwa namna ambavyo
ameyapokea maagizo wa Waziri Mpina , mmiliki wa kampuni ya Overland Bw.
Faisal Edha alisema kuwa amekubalina na maagizo ya Mpina na yupo tayari
kuendelea na uwekezaji na anaamini kuwa mkataba mpya utanufaisha pande
zote mbili.
Awali akipokea taarifa ya Mifugo
ya wilaya ya Handeni, Waziri Mpina alimpongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.
Godwin Gondwe kwa kuzitambua sheria za usimamizi wa mifugo na kuzitumia
jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kutokuwepo kwa uonevu kwa
watu wa jamii ya wafugaji na kuzitaka wilaya nyingine nchini kuiga mfano
wa wilaya hiyo kwa kuunda sheria ndogo ndogo zitakazowaongoza katika
sekta ya mifugo.