NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, JAPHET HASUNGA AMEIAGIZA TFS KUANZA MCHAKATO WA KUUNDA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA MISITU TANZANIA

December 23, 2017
1
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia)  akizungumza  na  Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu  Tanzania (TFS) makao makuu  jijini Dar es Salaam jana .  Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo
2
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (kulia)  akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto)  kuzungumza  na Watumishi wa TFS  makao makuu  jijini Dar es Salaam jana .
3
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania  (TFS) Dos Santos Silayo  akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga baada ya   kuzungumza  na  Watumishi wa  TFS makao makuu  jijini Dar es Salaam jana .
4
Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam.
5
Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam. (Picha na Lusungu Helela-MNRTBaadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam.
Picha na Lusungu Helela-MNRT
……………
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ianze mchakato wa kuandaa sheria ya kutoka Wakala kuwa   Mamlaka ya Usimamizi wa Misitu Tanzania ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa vile ikiendelea kubaki kuwa Wakala  kuna baadhi ya mambo itashindwa kuyashughulikia

 Wakala ni Idara za Serikali zilizoondolewa kwenye serikali kuu na zina nusu mamlaka na hazina mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake zenyewe.

 Amesema uanzishwaji wa Mamlaka hiyo itasaidia kupunguza migongano kati ya misitu iliyo chini ya   Tamisemi pamoja na vijiji kwa vile kutakuwa na Mamlaka moja ya kusimamia misitu tofauti na ilivyo sasa.

Ameyasema hayo jana wakati akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) makao makuu jijini Dar es Salaam

Amesema TFS kwa  hatua iliyofikia kwa sasa haistahili  kuwa Wakala kutokana na kazi kubwa iliyonayo hivyo inahitaji kuwa Mamlaka ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa uhuru zaidi.

Wakati akizungumza na Watumishi, Naibu Waziri Hasunga  amemtaka Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo  ahakikishe  katika mpango mkakati utakaoandaliwa hivi sasa  suala la uanzishwaji wa Mamlaka lipewe kipaumbele.

Katika hatua nyingine, Ameiagiza TFS iunde  chombo cha kusimamia na  kudhibiti ubora wa mazao ya misitu.

Amesema  chombo hicho kitakuwa kikipanga mazao ya misitu kulingana na ubora wake na sio kama sasa inavyofanyika mbao zozote zile zimekuwa zikiuzwa sokoni pasipo kujali  ubora wake.


Amesema  kuna changamoto ya bei za mbao sokoni na pia kuna changamoto ya ubora wa mbao zilizoko sokoni, Mbao nyingi zimetengenezwa  kwa miti ambayo  imevunwa ikiwa na  miaka sita au kumi ni lazima ubora wake uwe  hafifu.

‘’ Halafu unaenda kumshindanisha na mtu anayeuza mbao ambazo miti yake imevunwa ikiwa na  miaka 18 haziwezi  kushindanishwa  ubora kati ya mbao hizo lazima kiwepo chombo cha kuthibiti kama vile kwenye chakula kuna TFDA na kwenye bidhaa kuna TBS’’ alisema


 Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Hasunga amemtaka kila  mtumishi ahakikishe anapambana na rushwa kwa kumuagiza  Mtendaji Mkuu wa TFS  Prof.  Silayo  kuwahamisha watumishi pale inapotokea fununu kuwa mtumishi fulani anajihusisha na rushwa hata kama bado haijathibitika kwa vile fununu hizo haziwezi kuanza tu bila ya kuwa  harufu ya mazingira ya kupokea rushwa yanayotengenezwa.

Amesema katika suala la  ugawaji wa vitalu kuna vitendo vya rushwa vinafanyika kwani baadhi ya watu wanapewa vibali vya kuvuna kwa muda wa miezi minne lakini uvunaji ule unaendelea kwa  muda wa mwaka mmoja wakati  ilitakiwa kitalu hicho kivunwe kwa muda wa wiki mbili tu.’’ Alisema

 ‘’Mimi sikurupuki kwenye maamuzi yangu na sio kwamba nasema nimekuja kuwatumbua leo lakini nina taarifa nyingi kuhusiana na rushwa inavyotembea katika ugawaji wa vitalu’’

‘’Mtendaji ifanyie kazi taarifa hii  ya rushwa ila nikiona mambo hayaendi kama ninavyotarajia nitakuja kivingine. alisisitiza


 Katika hatua nyingine , Naibu Waziri Hasunga  ameiagiza TFS  iongeze ukusanyaji wa mapato kwa vile mapato yalipo sasa bado hayatoshelezi na yaliyokusanywa yatumike vizuri.‘’Taarifa nilizonazo kuna maeneo manne mapato  yanavuja paangalieni hapo mparekebishe ‘’  alisema

Wakati huo huo,  Hasunga ameiagiza TFS ianze kuwekeza katika maeneo ambayo inaona inaweza kuzalisha zaidi  kwa mfano  kwenye maporomoko ya Kalambo ili iweze kuongeza mapato

‘’Yale maporomoko ukikaa Zambia huwezi kuyaona vizuri ila ukikaa Tanzania unayaona vizuri’ tumieni fursa hiyo baada ya miaka miwili ijayo kinaweza kikawa kituo kikubwa cha utalii nchini.’’

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo amemhakikishia Naibu Waziri Hasunga  kuwa atatekeleza maagizo yake yote aliyoyatoa kwa maslahi mapana ya TFS.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »