ZAIDI YA BAJAJ 150 ZAMAKATWA WILAYANI KOROGWE KUTOKANA NA MAKOSA MBALIMBALI

December 07, 2017
ZAIDI ya Bajaji 150 zimekamatwa wilayani Korogwe mkoani Tanga kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo madereva kuendesha bila kuwa na leseni huku wakipakia abiria.
Ukamataji huo umefanyika wakati wa operesheni maalumu inayoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani hapa inayoendeshwa na Mamlaka ya Usimamizi wa vyombo vya majini na nchi kavu Sumatra mkoani Tanga.

Akizungumza jana,Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoani Tanga,Dkt Walukani Luhamba alisema bajiji hizo zilikamatwa wakati wa ukaguzi ambao waliufanya kuangalia iwapo madereva wanaendesha vyombo hivyo wana leseni.

Alisema lengo la operesheni hiyo ni kuhakikisha wanazibiti ajali
zisizokuwa za lazima kwa watumiaji wa vyombo hivyo ikiwemo kufuatwa kwa sheria za usalama barabarani.

“Katika operesheni hii tumekamata bajaji zaidi ya 150 ambao wameliki na madereva wamepewa onyo kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani na kutokurudia tena makosa yao “Alisema.

Aidha alisema pia licha ya kukamata bajaji hizo lakini pia walikamata pikipiki zaidi ya 170 ambapo kwenye Halmashauri ya Bumbuli walikamata pikipiki 60, Handeni Vijijini walikamata pikipiki 40 huku Korogwe wakikamatwa 70.

Hata hivyo alisema operesheni hiyo bado inaendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Tanga lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha watumiaji wanafuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zisizokuwa za lazima.

Ofisa Sumatra huyo pia alitoa onyo kali kwa wamiliki wa mabasi ya mikoa na wilayani kuacha kupandisha nauli katika kipindi hiki cha mwishoni mwa mwaka na watakaobainika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »