Waziri
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina akiwa na viongozi wa Mkoa wa
Kagera wa Serikali mara baada ya kuwasili jana kukagua shughuli za mifugo
katika Ranchi za Mifugo zilizopo mkoani hapo jana.
Waziri
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina(mwenye Kofia )akitoa maelezo ya
kwa mkuu wa Wilaya ya Richard Lugango kuboresha ulinzi katika Ranchi ya Kagoma
baada ya kumuamuru mwekezaji katika
Ranchi hiyo kuondoka mara moja baada ya kushindwa kutekeleza mkataba baina yake
ya Serikali hapo jana.
Waziri
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina akipima urefu wa bwawa la maji ya
kunyweshea mifugo katika Ranchi ya Kagoma mkoani Bukoba ambapo aliamuru
mwekezaji Agri Vision Global Ltd
katika Ranchi ya Kagoma mkoani Kagera kuondoka mara moja baada ya
mwekezaji huyo kushindwa kutekeleza mkataba huo katika kipindi cha miaka mitano
hapo jana.
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
akikagua eneo la ranchi ya Kagoma kuangalia hali halisi ya uwekezaji wa shamba la mifugo
hapo jana.
Waziri
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga
Mpina ameridhia maamuzi ya Kampuni ya Ranchi za NARCO kuvunja
mkataba baina ya mwekezaji Agri Vision Global Ltd katika Ranchi ya Kagoma mkoani Kagera na kuamuru aondoke mara moja
baada ya mwekezaji huyo kushindwa kutekeleza mkataba huo katika kipindi cha
miaka mitano.
Waziri
Mpina ametoa maelekezo hayo jana alipotembelea Ranchi ya Kagoma kuangalia
shughuli mbalimbali katika Ranchi hiyo
ambapo ametoa siku saba kwa mwekezaji huyo kuondoka katika eneo hilo na badala
yake Serikali kupitia NARCO kuendelea kusimamia shughuli za mifugo katika
Ranchi hiyo.
“Ninakuagiza Mkuu wa Wilaya kuanzia sasa
hakikisha unaimarisha ulinzi katika ranchi hii katika kipindi cha
kukabidhi Ranchi baina ya Serikali na Mwekezaji
ili kusitokee hujuma zozote” alisisitiza Mpina
Alitaja
baadhi ya mambo ambayo hayakutekelezwa na mwekezaji huyo kuwa ni pamoja na kujenga
machinjio ya nyama, kujenga
kiwanda, kutoa gawio la shilingi bilioni tatu kila mwaka katika kipindi cha
miaka mitano, kutoa shilingi 2672 kwa hekta moja kama tozo la ardhi na
kushindwa kuendeleza miundombinu ya NARCO waliyoikuta wakati wanaingia mikataba hiyo miaka mitano
iliyopita.
Waziri
Mpina amemuagiza Meneja Mkuu wa NARCO,
Profesa Philemoni Wambura kuhakikisha kwamba ndani ya siku saba
anampeleka Meneja katika Ranchi hiyo kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za ranchi
hiyo na kuhakikisha kuwa inafanya kazi zake kisasa.
Aidha
Mpina ametoa siku saba kwa Uongozi wa NARCO kuhakikisha kuwa imefanya
tathmini ya hasara zilizosababishwa na
mwekezaji huyo ili taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi yake ili aweze kuilipa Serikali ikiwa ni pamoja na
shilingi bilioni kumi na tano kama gawio
la miaka mitano iliyokaa ambalo amesema halijawahi kulipwa hata shilingi moja.
“Sasa
tumeamua kuchukua hatua na tutaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wawekezaji
wasiowaaminifu wanaotaka kuihujumu serikali katika sekta hizi za mifugo na
Uvuvi” alihoji Mpina
Alionya
wawekezaji kuacha tabia ya kuidanganya serikali kwamba wanauwezo wa kuwekeza
katika vitalu ili wapewe lakini wanabadili
matumizi baada ya kupewa.
Aliongeza kwamba
Serikali imegundua baadhi ya
wawekezaji wanaopewa vitalu wanawakodisha wafugaji kutoka nchi jirani na kujipatia faida wakati Serikali haipati chochote.
Awali, akipewa ripoti ya maendeleo ya mifugo na uvuvi
na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Deodatus Kinawiro mbaye ni Mkuu wa Wilaya ya
Bukoba alisema kutokana na operesheni za uvuvi haramu zinazoendelea wilaya ya
ngara imekamata tani 6 za samaki zilizokuwa zikipelekwa katika nchi ya burundi
.