
Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan 
akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa
 wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (Kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango 
Mhe. Dkt. Philip Mpango tayari kwa ufunguzi wa Kongamano la 8 la Mwaka 
la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi lililofanyika kwenye Kituo cha 
Kimataifa Cha Mikutano Arusha (AICC). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan 
akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa
 Ununuzi na Ugavi lililofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano 
Arusha (AICC). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Sehemu
 ya Wahudhuriaji wa Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na 
Ugavi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo 
lililofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa Arusha. (Picha na 
Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan 
akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya awali ya Heaven  
Moshono Arusha pamoja na walimu wao ambao walikuwa uwanja wa ndege wa 
Arusha wakati Makamu wa Rais anaondoka Arusha mara baada ya kufungua wa 
Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi lililofanyika 
kwenye Kituo cha Kimataifa Cha Mikutano Arusha (AICC). (Picha na Ofisi 
ya Makamu wa Rais)
Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan 
akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Mhandisi Binilith Mahenge 
mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitokea Arusha 
ambapo alifungua Kongamano la 8 la Mwaka la Wataalamu wa Ununuzi na 
Ugavi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
 













