Waziri
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) akiwa kwenye
picha pamoja na Viongozi wa Wilaya ya
Mvomero na Viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania alipotembelea ranchi ya Dakawa jana
Waziri
wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) akimsikiliza Mkuu
wa Wilaya ya Mvomero, Muhamed Utaly kulia
akitoa maelezo ya kuhusu eneo la hekta 20000 zilizoshindwa kuendelezwa
na mwekezaji Mtibwa Sugar kwa lengo la
ufugaji. Kushoto ni Meneja Mkuu wa
Kampuni hiyo bwana Stan Rau hapo jana.
Meneja
wa ranchi ya Mifugo ya Mkata, Iddi
Sadalah akimuonyesha Waziri wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina (mwenye Kofia) banda la Mbuzi
linalokadiriwa kuchukua mbuzi 800 kwa wakati mmoja katika ranchi ya
Mkata jana.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina
ameagiza Mtendaji Mkuu wa Ranchi za
Mifugo za Taifa, Profesa Philemoni Wambura kuvunja mikataba ya wawekezaji wa vitalu vyenye jumla
ya hekta 68,238 kwenye ranchi ya Mkata na Dakawa ndani ya mwezi mmoja baada kushindwa kuviendeleza vitalu vya ranchi na kushindwa kulipia kwa muda
mrefu.
Mpina
ameyasema hayo jana wakati alipotembelea katika ranchi ya Mkata na Dakawa kwa
lengo la kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika katika ranchi hizo.
Amezitaja
kampuni za wawekezaji ambazo zilizomilikishwa vitalu zinatakiwa kuvunja mkataba kwa kushindwa
kuendeleza upande wa ranchi ya Mkata katika Wilaya ya Kilosa kuwa ni pamoja na
Kadolo Farm Company Ltd kitalu namba 418
yenye hekta 4005,Bagamoyo Farm kitalu namba 419 yenye hekta 3672.96, A to Z
Animal Feeds Company Ltd kitalu namba 420 yenye hekta 3692.97 na Ereto
Livestock Keepers kitalu namba 422 yenye hekta 4020.54.
Katika
Wilaya ya Mvomero kampuni zilizoshindwa
kuendeleza vitalu ni pamoja na kampuni ya Overland kitalu namba 415 yenye hekta19446.28,
Katenda yenye hekta 2500, Mollel yenye
hekta 2500 na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa (Mtibwa Sugar) chenye hekta
20000 walizomilikishwa toka mwaka 1999 na kushindwa kukiendeleza na kukilipia kwa miaka 18.
Mpina
amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilosa kumaliza
mara moja migogoro inayoendelea baina ya wakulima na wafugaji. Aidha Waziri
Mpina amemtaka Diwani wa kata yaTwatwatwa, Katibu Tawala wa Halimashauri ya Wilaya ya Kilosa pamoja na
jamii ya wafugaji kumaliza migogoro inayowasumbua kwa muda mrefu kwa njia ya
mazungumzo kabla ya kukimbilia muhimili wa mahakama bila sababu yoyote.
Mpina
amesema kama vyombo vya Serikali vingetumika vizuri kuanzia ngazi
ya kijiji kungepunguza migogoro ya
wakulima na wafugaji katika wilaya hiyo. Wilaya ya Kilosa ni miongoni mwa Wilaya
zinaongoza kwa kuwa na migogoro mingi
baina ya wakulima na wafugaji hapa nchini.
Kwa upande mwingine, Waziri Mpina amezitaka Halimashauri
zote nchini kutotunga sheria kandamizi
dhidi ya wafugaji. Akitolea mfano, wa sheria ndogo ya Halimashauri ya Mvomero
ya kutoza faini ya shilingi 25, 000/=kwa kila mfugo kuingia katika Wilaya hiyo bila kufuata taratibu badala ya shilingi elfu kumi iliyoelekezwa
katika Sheria ya Magonjwa ya Wanyama
namba 17 ya Mwaka 2003.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) Magembe Makoye amesema upatikanaji wa ardhi
kwa ajili ya wafugaji kutasaidia kuondoa migogoro baina ya pande hizo na kuendelezwa kwa ranchi
hizo za taifa kutawasaidia wafugaji
kupata shamba darasa litakalo wasaidia kufuga kwa kisasa na kupata mbegu bora za mifugo.
EmoticonEmoticon