Mkongwe
katika mitindo nchini Tanzania na Marekani Mama wa mitindo Bi. Asya
Idarous Khamsin anatarajiwa kuonyesha mitindo yake mbalimbali ya ubunifu
wa mavazi katika sherehe ya maalum ya Watanzania itakayofanyika tarehe
9 Desemba,2017 huko Oakland California Nchini Marekani.
Kwa
mujibu wa Mama wa Mitindo, Bi. Asya Idarous Khamsin ameweka wazi kuwa,
onyesho hilo litakuwa la aina yake kwani watu watakaojitokeza
watashuhudia mitindo mipya kabisa ya mavazi ambauyo itaonyesha kwenye
jukwaa maalum siku hiyo sambamba na Chakula maalum cha kuchangia watu
wenye tatizo la ugonjwa wa Kansa nchini Tanzania.
“9
Desemba,2017 tumewaandalia onyesho maalum la mavazi. Watu wajitokeze
kwa wingi kushuhudia mavazi ya ubunifu. Pia kutakuwa na ‘fundraising
dinner’ ya kukusanya fedha kwa ajili ya (partnering to tackle cancer to
Tanzania) ambayo inafanyika kila mwaka.
Sherehe
hizo ni pamoja na kusherehekea Shamla shamla za Uhuru wa (Tanganyika)
ambayo sasa ni Tanzania” Alieleza Asya Idarous Khamsin.
Asya Idarous Khamsin
EmoticonEmoticon