Waziri Mpina katika Picha akivua samaki aina ya kambale alipotembelea Mradi wa mabwawa ya samaki wa Luhanga Wilayani Muleba.
Aliyeshika Samakai aina ya Sato ni Waziri Mpina alipotembelea Mradi wa Mabwawa ya Samaki wa Luhanga Wilayani Muleba.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Misenyi mara baada ya zoezi
la kutaifisha ng'ombe.
NA MWANDISHI MAALUM
MISENYI
Akiwa katika muendelezo wa ziara zake za operesheni kamata
mifugo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina Ameagiza kukamilisha
taratibu za Uhamiaji na Mahakama kupitia mwanasheria mkuu wa Serikali wa Wilaya
ya Misenyi Pamoja na Uhamiaji, ili kuweza kupigwa mnada kwa idadi ya ng’ombe
6648 walioingia nchini kinyemela toka nchi jirani ya Uganda na kukamatwa.
Waziri mpina alisema uvamizi wa kundi kubwa kama hilo la
wanyama linaweza kusabisha madhara makubwa katika mazingira kama vile
mmomonyoko wa ardhi, kuharibifu wa vyanzo vya maji, kumaliza malisho ya mifugo
iliyoko nchini, kusababisha migogogoro ya mara kwa mara kwa wakulima na
wafugaji na hata kuleta maambukizi ya magonjwa ya wanyama.
“Sisi kama Serikali hatuwezi kuruhusu hali hii iendelee na
mimi kama Waziri Mwenye dhamana nina jukumu la kuhakikisha tunalinda lasimali
hii ya malisho” Alisema Mpina.
Mpina alisema suala hili haliingiliani na Ushirika wa Afrika
Mashariki kwani Ushirika huo upo kisheria hivyo wavamizi wanaoingiza mifugo
kinyemela nchini toka nchi jirani ni wahalifu kama wahalifu wengine.
“Kwa hiyo naangiza ng’ombe hawa 6648 waliokamatwa hatua
ziendelee na ambao hawajakamatwa wakamatwe na wataifishwe na Serikali.”Alisisitiza
Waziri Mpina.
Kwa upande wa upande wake mkuu wa Wilaya ya Misenyi Kanali
Denis Mwila alisema kuwa zoezi la kutathmini ng’ombe katika wilaya yake bado
linaendelea na taratibu za kisheria zinafuatwa.
Alipokuwa Mkoani Kagera Mapema jana Mpina alitembelea mabwawa ya mradi wa samaki yaliyopo Wilayani Muleba katika kijiji
cha Luhanga na kusema Serikali ina nia ya kukomesha kabisa uvuvi haramu ikiwa
ni pamoja na kuwasaka wavuvi haramu kule waliko na kuwa na nyenzo.
Aidha, akiwa Bukoba Mjini Mpina alitembelea kiwanda cha
kuchakata samaki cha Suprime Fish Ltd na kuagiza wamiliki wa viwanda vya samaki
nchini kuhakikisha wanachukua hatua za haraka kufufua viwanda hivyo na kuongeza
uzalishaji kwani Serikali imeshaanza kuchukua hatua ya kuhakikisha samaki wanapatikana
kwa wingi nchini.
EmoticonEmoticon