DKT.KIGWANGALLA:“SASA TUTAKAMATA MAJANGILI KULIKO KUKAMATA NYARA

October 30, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamisi Kigwangalla ameweka wazi kuwa moja ya mikakati ya Wizara yake hiyo ni kuhakikisha wanachukua hatua za haraka katika kulinda rasilimali za Taifa kwa kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili nchini.
Dkt. Kigwangalla amesema hayoi mapema leo mjini Dodoma wakati wa akielezea namna walivyojipanga kukamata majangili kabla hawajhafanya ujangili.
“Tumekusudia kukamata majangili kabla hawajafanya ujangili kuliko kukamata nyara. Tutaisambaratisha na kuifumua kabisa mitandao ya biashara haramu ya ujangili nchini. Ameeleza Dkt.Kigwangalla
Aidha, ameendelea kutuma salamu kwa majingili wote kuachana na baishara hiyo kwa kujisalimisha ama kukimbia kwani kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa mtandao mpana wa majingili.
“Jana tumefanikiwa kumkamata Ndg. Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu, akijipanga kuelekea Moru, ndani ya hifadhi ya Serengeti kwa malengo ya kuua Faru. Amekutwa na risasi 356, magazines 2, msumeno mdogo na mafuta ya kusafishia silaha. Wizara yangu imejipanga na tutaendelea kutumia mbinu za kisasa zaidi za intelijensia kudhibiti ujangili huu” alimalizia Dkt.Kigwangalla.
Dkt.Kigwangalla amebainisha kuwa, tayari vikosi maalum kwa kushirikiana na Wizara yake wakiwemo wale wa Wanyama pori wanaendelea na uchunguzi wa ndani hasa katika mitandao ya Majangili wakubwa wa ndani na nje ya Nchi.
Ndg. Masalu Wella Nangale wa kijiji cha Mwasengela, Meatu aliyekamatwa akijipanga kuingia Hifadhi ya Serengeti 
Baadhi ya risasi zilizokamatwa na jangili huyo  
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangalla akiwa pamoja na Mhifadhi wa Mkuu wa Serengeti William Mwakilema pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro wakiangalia mpaka unahishia pori tengefu la Loliondo-Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti mwishoni mwa wiki wakati wa kukagua maeneo hayo yenye mgogoro na wafugaji.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »