Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi
Lugola akishiriki katika zoezi la uzinduzi wa operesheni maalumu ya
usafi nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Tandale jijini Dar
es salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi
Lugola akishiriki katika zoezi la uzinduzi wa operesheni maalumu ya
usafi nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Tandale jijini Dar
es salaam.
Zoezi la usafishaji wa mitaro likiendelea katika eneo la Tandale kwa Ali
Maua, maeneo hayo yameathirika kwa kiasi kikubwa na mvua za hivi
karibuni kutokana na kurundikana kwa taka ngumu.
Sehemu ya Mto Ng'ombe kama unavyoonekana ukiwa umekithiri kwa taka. Hii
leo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira
Mhe. Kangi Lugola (hayupo pichani) ameshiriki katika uzinduzi wa
Operesheni maalumu ya kusafisha mazingira kote nchini. Zoezi la uzinduzi
wa usafi limefanyika katika Mto Ng'ombe.
Harakati mbalimbali
zimekuwa zikifanyika ili kuweka Majiji, Halmashauri na Miji, yetu safi, ikiwa ni pamoja na matamko mbalimbali ya
viongozi wakuu hapa nchini. Aidha, Halmashauri za miji na majiji zimekuwa
zikiendesha kampeni za usafi kwa kuweka siku maalumu za kufanya usafi wa mazingira
na pia kusimamia sheria, kanuni, miongozo na sheria ndogo izinayohusu mazingira.
Nguvu za ziada
zinahitajika ili Halmashauri ziweze kuchukua hatua za dhati za kudhibiti taka
pamoja na kuhakikisha sheria ndogo na sheria nyingine zinatekelezwa kwa vitendo
ili kuhakikisha usafi wa mazingira unasimamiwa
ipasanyo na kuhakikisha mazingira yanayotuzunguka yanakuwa masafi.
EmoticonEmoticon