Elias
Kwandikwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri,
wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa
kiwango cha lami, mkoani humo.
Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze
akitoa taarifa ya mradi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, alipokagua ujenzi wa
barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias
Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri anayesimamia ujenzi wa
barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha lami. Kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri,
Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze
akifurahi jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwamri, wakati wa
ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28 kwa kiwango cha
lami, mkoani humo.
Mitambo ya ujenzi ikiwa eneo la kazi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kaliua-Urambo KM 28, mkoani Tabora.
……………
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa
Elias Kwandikwa (Mb), ametoa wito kwa madiwani nchini kuanisha barabara
zote zenye kipaumbele katika maeneo yao ili ziweze kuingizwa kwa urahisi
kwenye mpango wa matengenezo.
Kwandikwa
ametoa wito huo mkoani Tabora wakati akikagua ujenzi wa barabara ya
Kaliua-Urambo yenye urefu wa KM 28 ambapo pamoja na mambo mengine
amesema mapendekezo yao yawasilishwe katika kamati za maendeleo za
wilaya, mikoa na bodi za barabara.
“Unakuta
diwani analalamika kwamba barabara haijatengenezwa ama haifikiliwi
kutengenezwa lakini ukija kufuatilia unakuta hakuna mahali popote ambapo
taariza za barabara hiyo kutengenezwa zimewasilishwa”, amesema Mhe.
Kwandikwa.
Amesisitiza
kuwa umuhimu wa kupeleka mapendekezo hayo kutasaidia barabara hizo
kutambulika na kuondoa malalamiko kwa wananchi na baadhi ya viongozi kwa
kuwa zitaingizwa katika mipango ya ujenzi kwa wakati.
Kuhusu
barabara hiyo ya Kaliua-Urambo inayojengwa kufuatia agizo la Rais Dkt
John Magufuli, Mhe. Kwandikwa amemtaka mkandarasi kuhakikisha ujenzi huo
unafanyika kwa kuzingatia viwango vya ubora uliopangwa kwa mujibu wa
mkataba wake.
“Lengo
la mheshimiwa rais ni kurahisha huduma ya usafiri na usafirishaji kwa
wananchi hivyo mkandarasi huna budi kufanya kazi hii haraka na kw
kuzingatia makubaliano ya mkataba wako.Amesema waziri kwandika.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwamnri, amemuhakikishia Naibu
Waziri Kwandikwa kuwa serikali ya mkoa huo imejipanga kushirikiana na
mkandarasi ili barabara hiyo ikamilike ndani ya muda uliopangwa.
“Kwanza
sisi kama mkoa tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuona umuhimu wa
kutuwekea lami katika barabara hii kwa sababu itaongeza ufanisi kwa
wananchi kufanya shughuli zao kiurahisi”, amesema Mwanri.
Naye
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian
Ndibalinze amesema kuwa Wakala utawasimamia makandarasi wazawa Samota
Construction, Anam Roads Works na Jossam Contractor (JV) ili kuhakikisha
wanamaliza ujenzi huo kwa wakati baada ya changamoto ya tatizo la maji
kupatiwa ufumbuzi.
Naibu
Waziri Mhe. Elias Kwandikwa, yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua
ujenzi wa barabara na madaraja katika mikoa ya Singida, Tabora na
Kigoma.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
EmoticonEmoticon