NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA NISHATI SUBIRA MGALU AWAHAKIKISHI WAKAZI WA MBAGALA UMEME WA UHAKIKA

October 20, 2017

Mhandisi Emanuel Manlabona akimuonyesha  Naibu Waziri Nishati Subira Mgalu Juu ya uwezo wa kituo hicho cha kusambaza umeme kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Usafirishaji Umeme Mhandisi Bishaija Kahitwa
Mhandisi Emanuel Manlabona akimuonyesha  Naibu Waziri Nishati Subira Mgalu Juu ya uwezo wa kituo hicho cha kusambaza umemekulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Usafirishaji Umeme Mhandisi Bishaija Kahitwa
Naibu  Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu kulia akisalimiana na mkazi wa Mbagala
Naibu  Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu amewahakikishia wakazi wa Mbagala umeme wa uhakika  kwani wizara ya nishati kwa kushirikiana na  wataalamu mbalimbali wa TANESCO wanafanya jitihada za kutosha kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana ili kuwezesha matumizi ya viwanda mbalimbali vilivyopo mbagala na matumizi ya Nyumbani kwa wakazi wa mbagala.
“Tumesikia matatizo yenu yanayohusiana na Umeme, ila Napenda kuwahakikishiani kuwa  Wizaraya Nishati pamoja na TANESCO kwa ujumla tunafanya kazi, kuhakikisha umeme mbagala unakua wa Uhakikia, leo hapa nimekuja kutembelea hiki kituo cha usambazaji umeme cha mbagala , ambacho kinajengwa na kwa kushirikiana kwa pamoja, tunapambana kituo hichi kikamilike ndani yam waka huu mpaka kufikia disemba , kituo hichi kiwe kimekamilika. “

Hayo aliyazungumza  jana katika ziara aliyoifanya katika  vituo vya kusafirisha umeme, kituo cha mbagala na kurasini lengo kubwa ikiwa ni kuangalia hali halisi ya utendaji wa TANESCO katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma hii ya Nishati ya umeme wa Uhakika.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »