Na Mwandishi Wetu
MKAZI wa Mikumi mkoani Morogoro, Frank
Chodaus amekuwa ni mmoja wa wanaonufaika na mchezo wa kubashiri matokeo kutoka
kampuni ya Sokabet baada ya kujishindia shilingi milioni 2 baada ya kubashiri
kwa kutumia shilingi 1000 tu.
Ndani ya tovuti ya kampuni hiyo ya
Sokabet kila wiki huwa kuna kipengele kinachowawezesha washiriki kushinda hadi
shilingi milioni 100 kwa kubashiri matokeo kwa shilingi elfu moja tu, ambapo
ndipo huko Frank aliponufaika.
Akizungumza juu ya ushindi huo
mratibu wa Kampuni ya Sokabet, Franko Ruhinda alisema mshindi huyo alipatikana
wikiendi iliyopita baada ya kupatia michezo 11 kati ya 13 ambayo alitakiwa
kupatia kwenye kipengele hizo cha Jackpot.
“Unajua kama ambavyo tumekuwa
tukishauri watu kuendelea kujiunga na kushiriki katika Sokabet, ndani ya muda
mfupi wanaweza kujiingizia mamilioni kwa kuweka fedha kidogo tu katika ubashiri
wao, ushindi wa Frank ni mfano tu wengi wanaojishindia ndani ya tovuti yetu,”
alisema Franko.
Alipowasiliana na mwandishi wa habari
hii, mshindi huyo alisema ilikuwa ni furaha kwake kupata fedha hizo kwa kuwa
hakutegemea lakini ni jambo muhimu kwa kuwa fedha hizo zimemwezesha kutatua
matatizo yake mengi.
Akifafanua zaidi alisema: “Mimi ni
fundi magari na nimekuwa nikishiriki sana katika michezo hii ya kubet, sasa
Sokabet ilivyoanzishwa kwanza sikujiunga kwa kuwa nilikuwa sijapata elimu
vizuri, baada ya kufatilia magazeti ndipo nikawajua vizuri na kujiandikisha.
“Nilipojiandikisha
nikaanza kubet mdogomdogo, mwanzoni sikupata, lakini kila wiki nimekuwa nikibet
katika vipengele tofauti kikiwemo kipengele cha Jackpot.
“Sasa wiki iliyopita, nilibet kama
kawaida kwa buku (Sh 1,000), baada ya hapo nikaendelea na shughuli zangu,
sikufuatilia majibu kwa kuwa mechi nyingi ziliisha usiku wa Jumamosi.
“Kawaida huwa nikibet kama hivyo
nasubiri kuona kama nitapata ujumbe, nikiona sijapata dnipo nafungua akaunti
yangu ya kubet na kuangalia nilipokosea,
“Sasa Jumapili nikashtukia nikipata
ujumbe kuwa nimeshinda shilingi milioni 2, ilikuwa furaha kubwa kwangu kwa kuwa
sikutegemea na unajua wakati mwingine hivi vitu ni bahati.”
Aliongeza kwa kusema haya: “Hicho
kipengele mtu anatakiwa kupatia michezo 13 ambapo kama ningefanikiwa hivyo
maana yake ningepata milioni mia, na kama ningepatia michezo 12 ningepata
milioni tano, ila mimi nilipatia michezo 11.”
Kuhusu matumizi ya fedha hizo, fundi
huyo ambaye ana umri wa miaka 25 alisema zilimsaidia katika matumizi yake
lakini ataendelea kubet kwa kuwa anaamini anayo nafasi nyingine ya kupata mzigo
mkubwa zaidi ya alioupata mwanzo.
EmoticonEmoticon