IAWRT yavitaka vyombo vya habari nchini kuwa na sera ya jinsia

October 20, 2017
Chama cha Kimataifa cha Wanawake Wanaofanyakazi kwenye Vituo vya Runinga na Redio (IAWRT) imevitaka vyombo vya habari kuwa na sera ya jinsia kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza ufanisi wa kazi katika vyombo hivyo. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa IAWRT nchini, Rose Mwalimu katika mafunzo yaliyotolewa na chama hicho kwa waandishi wa habari wa vituo vya runinga, redio na mtandaoni kuhusu sera ya jinsia katika vituo vyao vya kazi. Mwalimu alisema katika kusaidia kuwepo na sera ya jinsia wameandaa mafunzo hayo ambayo yanalenga kusaidia kukuza sera ya jinsia katika maeneo ya kazi kwa wanahabari jambo ambalo litasaidia kuboresha vipindi vinavyorushwa kwani hata uandaaji wake utakuwa unahusisha jinsia zote. Chama cha Kimataifa cha Wanawake Wanaofanyakazi kwenye Vituo vya Runinga na Redio (IAWRT) nchini, Rose Mwalimu akizungumza katika mafunzo ya waandishi wa habari yaliyoandaliwa na chama hicho. "Haya mafunzo ya leo ni njia mojawapo ya kukuza sera ya ujinsia katika vyombo vya habari, utekelezaji wake huwa ni katika kutafuta watu ambao ni watangazaji ambao wao ndiyo watakuwa kama wasimamizi ambapo kupitia wao watatengeza vipindi ambavyo vitakidhi sera ya jinsia inavyotaka ili na wengine waige, "Lengo ni kuwa na vipindi bora na sio tu vipindi bora lakini vipindi bora ambavyo vitakuwa na tija katika jamii ... tatizo wafanyakazi wengi hawajui haya madhara kama hakuna utekelezaji wa sera ya jinsia, madhara yapo kwa namna mbili, kwa wafanyakazi wao wenyewe na kwa wasikilizaji na watazamani, kwako kutokuwa na sera kama hushirikihi hizi jinsi mbili hata huo uhuru wa kupeana habari unakuwa haupo," alisema Mwalimu. Alisema kuwa takwimu za utafiti walioufanya mwaka 2014 zinaonyesha kuwa ni vyombo vya habari vichache ambavyo vina sera ya jinsia hivyo hata uwiano wa madaraka katika vyombo hivyo unakuwa upande mmoja wa wanaume. “Utakuta hata vyombo vya habari wakurugenzi na wahariri wakuu ni wanaume sasa wanawake wapo wapo na wanafanya nini?, wanawake wengi watangazaji wanapewa habari zinazowahusu wao wenyewe lakini hawashirikishwi vya kutosha katika habari za maendeleo," alisema Mwalimu.
Gladness Munuo akiwasilisha mada mbalimbali katika mafunzo kwa wanahabari kuhusu sera ya jinsia.
Baadhi waandishi wa habari walioshiriki mafunzo kuhusu sera ya jinsia.
Washiriki katika picha ya pamoja.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »