MAADHIMISHO YA JUBILEE YA MIAKA 50 YA SHULE YA SEKONDARI SHINYANGA YAFANYIKA SHINYANGA

October 14, 2017
Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Shule ya Sekondari Shinyanga “Shy Bush” iliyopo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Oktoba 13,2017.
Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya shule hiyo kongwe mkoani Shinyanga yameenda sambamba na mahafali ya 51 ya Kidato cha nne katika shule hiyo ambapo jumla ya wanafunzi 101 wanahitimu elimu yao ya sekondari mwaka huu.
Mgeni rasmi alikuwa  Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei kwa niaba ya wanafunzi mbalimbali waliosoma katika shule hiyo.
Jubilee hiyo pia imehudhuriwa pia na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack,walimu wakuu waliowahi kusoma katika shule hiyo,wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo,wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo,taasisi,mashirika na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga.
Maadhimisho hayo yameenda sanjari na Harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba mbili za walimu kila mmoja ikiwa na uwezo wa kubeba familia tano,ujenzi wa jengo la wanafunzi wenye mahitaji maalum na ujenzi wa jengo la maabara ya zahanati na vyumba vya kupumzikia wagonjwa.
Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 20.5 na mifuko 465 ya saruji imepatikana huku wadau na wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo wakiombwa kupeleka michango yao ili kukamilisha ujenzi wa majengo hayo pamoja na kusaidia mahitaji yanayotakiwa katika shule hiyo.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Shule ya Sekondari Shinyanga na mahafali ya 51 ya kidato cha nne mwaka huu katika shule hiyo.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Zainab Telack akizungumza katika maadhimisho hayo ambapo aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo yao shuleni na kutumia vizuri mitandao ya kijamii badala ya kuangalia vitu visivyowasaidia katika masomo yao. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Zainab Telack akizungumza katika maadhimisho hayo ya miaka 50 ya shule ya sekondari Shinyanga na mahafali ya 51 ya kidato cha nne katika shule hiyo. 
Awali Vijana wa skauti wakicheza mchezo wa kutembelea kwa kutumia kamba juu ya mti wakati wa Jubilee ya miaka 50 ya Shule ya Sekondari Shinyanga 'Shy Bush' na mahafali ya kidato cha nne mwaka 2017.
Vijana wa skauti wakiruka 
Kulia ni Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei na Mkuu wa Shule ya Sekondari Shinyanga,Deusdedith Malelemba wakielekea katika majengo ya watumishi yanayoendelea kujengwa katika shule hiyo kwa ajili ya kuweka jiwe la msingiJengo kwa ajili ya watumishi wa shule ya sekondari Shinyanga linaloendelea kujengwa ambalo limewekewa jiwe la msingi leo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Shinyanga,Deusdedith Malelemba akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei kuhusu ujenzi wa nyumba za watumishi katika shule hiyo
Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei akiweka jiwe la msingi katika moja ya majengo yanayoendelea kujengwa katika shule hiyo
Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei baada ya kuweka jiwe la msingi
Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei akipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya Sekondari Shinyanga aliyosoma 
Mwalimu mkuu wa kwanza katika shule ya Sekondari Shinyanga, Profesa Geofrey Mmari akipanda mti katika shule hiyo. Profesa Mmari ndiye mwanzilishi wa kampeni ya upandaji miti katika shule hiyo kuzungukwa na msitu 
Mwalimu mkuu wa kwanza katika shule ya Sekondari Shinyanga, Profesa Geofrey Mmari akipanda mti 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akiwasili katika ukumbi palipofanyika Jubilee ya miaka 50 ya Shule ya Sekondari Shinyanga na mahafali ya 51 ya kidato cha nne katika shule hiyo
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Stephen Magoiga,akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack,Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei na Mkuu wa Shule ya Sekondari Shinyanga,Deusdedith Malelemba.
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Shinyanga wakiwa ukumbini
Wanafunzi wa kidato cha nne wakiwa eneo la tukio 
Mwenyekiti wa Bodi ya shule akitoa neno 
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Shinyanga wakisoma risala kwa mgeni rasmi 
Wachezaji wa ngoma ya Igembe Sabho kutoka wilayani Kishapu wakitoa burudani wakati wa mahafali hayo 
Mwalimu mkuu wa kwanza katika shule ya Sekondari Shinyanga, Profesa Geofrey Mmari akitoa neno wakati wa Jubilee hiyo ya miaka 50 ya shule ya Sekondari Shinyanga.
Wageni waalikwa wakiwa katika eneo la tukio 
Mwalimu mkuu mwingine wa shule ya Sekondari Shinyanga,Zephania Masaki aliyeitumikia shule hiyo kuanzia mwaka 1979 - 1989 akitoa neno 
Wanafunzi wa kidato cha sita katika shule hiyo wakifuatilia kinachoendelea eneo la tukio 
Wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio 
Wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tatu wakiwa katika eneo la tukio 
Wanafunzi wa kidato cha tano na sita wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea 
Wanafunzi wakifuatilia matukio 
Wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo 
Wanafunzi na walimu waliowahi kufundisha na kusoma katika shule hiyo 
Mwalimu mkuu mwingine aliyewahi kuitumikia shule hiyo Wilson Mbanga akitoa neno ambapo aliwataka wanafunzi kushirikiana na walimu wao ili kufikia malengo yao 
Mmoja wa wanafunzi waliosoma katika shule ya sekondari Shinyanga (1989-1991) Sabasaba Kitewita,ambaye sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB akitoa neno wakati wa maadhimisho hayo
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mwanafunzi mwingine aliyesoma katika shule ya Sekondari Shinyanga ,(1981 - 1984), Mang'era Mang'era ambaye sasa ni Afisa Mipango wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu akitoa neno wakati wa maadhimisho hayo ya miaka 50 ya shule hiyo
Mwanafunzi mwingine aliyesoma katika shule hiyo mwaka 1990-1992,Msiandi Samwel ambaye sasa ni Mwekezaji wa ufugaji wa samaki na usindikaji wa samaki akitoe neno
Wageni mbalimbali wakifuatilia maadhimisho hayo
Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Nyabaganga Talaba akizungumza katika maadhimisho hayo ya miaka 50 ya shule ya sekondari Shinyanga
Walimu na wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiendesha harambee ya kuchangia maendeleo ya shule ya sekondari Shinyanga
Mgeni rasmi Philip Alfred Magani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Tanzania,Dkt. Charles Kimei akionesha kitita cha shilingi milioni 5 zilizotolewa na Dkt. Kimei kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya shule hiyo 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akihesabu pesa zilizotolewa na wadau
Harambee inaendelea
Wanafunzi wakiwa eneo la tukio
Zoezi la uchangiaji damu pia linaendelea
Harambee inaendelea
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akionesha fedha zilizotolewa na wadau
Harambee inaendelea
Wanafunzi waliosoma katika shule ya sekondari Shinyanga miaka ya nyuma wakiwa eneo la tukio
Wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio
Wanafunzi wakiombewa na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kwa ajili ya mtihani unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni
Mwanafunzi akiimba wimbo
Wanafunzi wakitoa burudani ya wimbo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Shinyanga,Deusdedith Malelemba akisoma risala ya shule kwa mgeni rasmi
Mgeni rasmi akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne 2017
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea
Picha ya pamoja,mgeni rasmi viongozi mbalimbali na wanafunzi wa kidato cha nne 
Picha ya pamoja,mgeni rasmi viongozi mbalimbali na wanafunzi wa kidato cha nne 
Picha ya pamoja,mgeni rasmi viongozi mbalimbali na wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo
Picha ya pamoja,mgeni rasmi viongozi mbalimbali na viongozi wa serikali ya wanafunzi katika shule hiyo
Picha ya pamoja,mgeni rasmi viongozi mbalimbali na waandaaji wa Jubilee hiyo
Picha za kumbukumbu zikaendelea kupigwa
Mc Mama Sabuni naye akapiga picha mgeni rasmi viongozi mbalimbali
Picha zikaendelea kupigwa
Picha ya pamoja,mgeni rasmi viongozi mbalimbali na viongozi wa madhehebu ya dini
Picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »