Muwasilishaji wa mada katika kongamano lililowajumuisha Wasichana wanaosoma kidato cha tano na sita katika shule mbalimbali mkoani Kilimanjaro,Nyamagesa Laban akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika Chuo cha Wanyamapori Mweka.
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa karibu ujumbe uliokuwa ukitolewa na Nyamagesa ambaye pia ni mwandishi wa vitabu.
Baadhi ya wananfunzi walioshiriki kongamano hilo wakiuliza maswali kwa Nyamagesa mara baada ya kumaliza kutoa ujumbe kwa wanafunzi hao.
Muwasilishaji wa mada katika kongamano la Wasichana wa Shule za Sekondari mkoni Kilimanjaro,Stumai Simba akizungumza katika kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia Mada zilizokuwa zikitolewa.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
WASICHANA walioko shuleni wametakiwa kuacha kuchagua kazi za kufanya
pindi wamalizapo masomo na badala yake wafanye maandalizi ya kujiajili kwa kufanya
shughuli za ujasiliamali wakati wakiendelea na harakati za kutafuta kazi.
Mbali na hayo wasichana pia wametakiwa kujenga tabia ya
kujiamini na kuacha tabia ya kuwa tegemezi ili kuondokana na mfumo uliopo
katika jamii kwa sasa ya kuwa mtoto wa kike ni wa kuwezeshwa na kuhurumiwa.
Hayo yameelezwa na wawezeshaiji wakati wa kongamano lililofanyika
katika Chuo cha Wanyapori (Mweka) na kuandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali
la Africaid kupitia mradi wake wa KISA na kukutanisha zaidi ya wanafunzi 1400
kutoka shule 11 za mkoa wa Kilimanjaro .
Stumai Simba ni miongoni mwa wasichana walioamua kujiajiri
na baadae wanatumika katika kutoa hamasa kwa wasichana hasa wanaojiandaa
kuhitimu masomo yao ya ngazi ya sekondari kushiriki kuondoa mfumo dume katika
jamii amewataka wasichana kutokata tamaa.
Msimamizi wa Mradi wa KISA mkoa wa Kilimanjaro ,Devota Mlay
amesema lengo la kuwakutanisha wanafunzi wa kike wanaosoma kidato cha tano na
sita ni kuwaandaa kwenda kutoa elimu kwa mtoto wa kike katika jamii pindi
wamalizapo masomo .
Kwa upande wa wanafunzi walioshiriki kongamano hilo
wameeleza mambo wanayojifunza kupitia makongamano huku wakifurahishwa na namna
ambavyo wawasilishaji wa mada walivyofanikiwa bila ya kungojea kupata ajira
serikalini.
Kongamano hilo ambalo limejumisha shule za 11 kutoka wilaya
za Mwanga,Rombo,Same,Siha ,Hai na Moshi
mjini linatarajia pia kufanyika katika mkoa wa Arusha na kuhusisha wanafunzi wa
kidadto cha tatno na sita katika shule za mkoa wa Arusha.
EmoticonEmoticon