Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya
Maliasili na Utalii hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla
amewataka watanzania kuendelea kumuombea dua pamoja na ushirikiano
katika majukumu yake mpya.
“Nimepokea
salamu nyingi za pongezi na shukrani kwa Mungu aliye juu. Sintoweza
kumjibu kila mtu, uungwana ni kutambua pongezi zenu na dua tele
mlizotuombea, nawashukuru sana ndugu zangu. Tuzidi kuombeana dua tu.
Tuna
kazi ngumu ya kukimbia kukidhi matarajio ya kiongozi wetu Mkuu
aliyetuamini na matarajio ya wananchi wenzetu. Binafsi nawaahidi nyote
kuwa sintowaangusha! Ahsanteni sana ndugu zangu, natarajia ushirikiano
wenu wa kila hali.” Alieleza Dk. Hamisi Kigwangalla.
Awali
taarifa za kuteuliwa kwake katika wizara nyingine, alizipata kupitia
kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi kwa njia ya simu wakati akiwa kwenye
majukumu ya ziara ya kuboresha mfumo wa afya, akiwa Wilayani
Nachingwea, Kata ya Kilimalondo umbali wa zaidi ya kilometa 100, kutoka
Makao makuu ya Wilaya hiyo ya Nachingwea, aliweza kusitisha ziara yake
hiyo ambayo alitakiwa kuendelea katika Vijiji na Wilaya nyingine ya
Liwale.
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Utalii
hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua chumba cha
upasuaji mkubwa cha kituo cha AAfya Kilimalondo, Wilayani Nachingwea
Mkoani Lindi.
Dk.Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa kituo cha Afya Kilimalondo wakati wa ziara hiyo
Mbunge
wa Nzega Vijijini ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kabla ya uteuzi mpya wa Wizara ya Utalii
hiyo jana Oktoba 7,2017, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa vipya vya
chumba cha upasuaji mkubwa cha kituo cha AAfya Kilimalondo, Wilayani
Nachingwea Mkoani Lindi. Kituo hicho kilifungiwa kisifanye upasuaje
mpaka kitakapokidhi vigezo, hata hivyo Dk.Kigwangalla alitoa miezi
mitatu kiwe kimefanyiwa marekebisho na kianze kazi mara moja
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Lindi akimpatia taarifa Dk. Kigwangalla juu ya
uteuzi wake mpya hivyo kusitisha shughuli zote zilizokuwa zimepangwa
kuendelea katika wilaya hiyo.
Dk.Kigwangalla
akiagana na viongozi wa Wilaya ya Nachingwea baada ya kusimamisha
ziara yake kufuatia uteuzi mpya. Baada ya kupata taarifa hiyo kila kitu
ilibidi kisimame hapo hapo. Namba za NW AMJW ilibidi ziondolewe na
safari ya kutoka huko ianze.
Dk.
Kigwangalla akiwa Mhe. Hassan Elias Masala (Mb.), Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea wakiagana mapema jana Oktoba 7,2017, majira ya saa nane za
mchana baada ya kupata ujumbe wa kuteuliwa nafasi mpya. Hiyo ni baada ya
kumaliza kazi kituoni hapo Kilimalondo na kuanza kuelekea Liwale,
Kituo cha Afya Kibutuka, Ndipo alipopata taarifa kuna mabadiliko ya
Baraza la mawaziri.
Awali
kabla ya kupata taarifa za majukumu mapya, Dk. Kigwangalla alikuwa
aendelee na ziara hiyo katikaWilaya ya Liwale, Kituo cha Afya Kibutuka.
Dk.
Kigwangalla alikuwa katika ziara yake hiyo ya kikazi ya siku tano ndani
ya Mkoa wa Lindi ambapo alitoa maagizo mbalimbali ya kuhakikisha
viongozi wa Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali wanatekeleza maagizo
yote aliyotoa kwani ni maagizo halali ya kiserikali na watakaoshindwa
watachukuliwa hatua. Miongoni mwa maagizo hayo ni pamoja na kila kituo
cha Afya kuhakikisha kina chumba cha upasuaji kufuatia agizo/tamko la
Mwandoya alilolitoa Novemba 2016, Mwandoya Meatu Mkoani Simiyu.
EmoticonEmoticon