MAHAFALI YA KWANZA YA DARASA LA SABA NA PRE - UNIT SHULE YA LITTLE TREASURES SHINYANGA YAFANA

October 08, 2017

Jana Jumamosi Oktoba 7,2017 kumefanyika mahafali ya kwanza ya Darasa la Saba katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.
Mbali na kufanyika kwa mahafali hayo ya darasa la saba pia kumefanyika mahafali ya sita ya darasa la awali (Pre Unit) sambamba na uzinduzi wa Bendera na Wimbo wa shule hiyo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wazazi na wadau mbalimbali wa elimu alikuwa Saleh Shaban Mohammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Salum Hamis Salum maarufu “Salum Mbuzi”.
Akizungumza katika mahafali hayo, Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic alisema shule hiyo yenye mchepuo wa Kiingereza ilianzishwa Julai mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi 12 na kwamba mwaka huu ndiyo mara yao ya kwanza kufanya mahafali wakiwa na wahitimu 35.
“Tulianza na wanafunzi 12 katika chumba cha gereji huko Mwasele,leo shule ina jumla ya wanafunzi 622,waliohitimu mwaka huu ambao tunawafanyia mahafali ni 35,hii ni hatua nzuri tunamshukuru Mungu na wazazi ambao wamekuwa bega kwa bega nasi kuhakikisha shule hii inafanikiwa”,alieleza Dominic. 
Naye Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita aliipongeza bodi ya shule, walimu,wafanyakazi wa na wazazi kwa ushirikiano walionao katika kuhakikisha kuwa shule hiyo inatoa elimu bora kwa wanafunzi. 
Katika hatua nyingine Mwita alisema ili kuinua kiwango cha elimu,wameanzisha ujenzi wa shule ya sekondari na wanafanya jitihada mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanapata usajili ili shule ianze kupokea wanafunzi kuanzia mwaka 2018. 
Aidha aliwaomba wazazi na wadau wa elimu kuendelea kutoa ushirikiano katika kukamilisha ujenzi unaoendelea wa jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” . 
Akitoa hotuba yake,mgeni rasmi Saleh Shaban Mohammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products aliipongeza shule hiyo kuendelea kutoa elimu bora na kuwa na mazingira bora ya kujifunzia hali inayosababisha watoto wakue vyema kiakili,kimwili na kimaadili. 
“Msingi mzuri wa elimu kwa mtoto ni kuanzia shule ya msingi hivyo nawasihi wazazi kupeleka shule,serikali yetu inapigania viwanda,viwanda hivi vinahitaji rasilimali watu,lazima tuwapatie elimu hawa watoto wetu ili maarifa wanayopata wayatumie katika viwanda hivi”,aliongeza. 
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo kwenye Mahafali hayo ametusogezea picha za matukio yaliyojiri…Tazama hapa chini
Hapa ni katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza ya Darasa la Saba na mahafali ya sita ya darasa la awali (Pre Unit) yaliyofanyika leo Jumamosi Oktoba 7,2017
Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic akizungumza katika mahafali hayo
Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Wazazi na walezi wakiwa katika mahafali hayo
MC Kifagio akikoleza neno kwa Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita
Mgeni rasmi bwana Saleh Shaban Mohammed kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products,Salum Hamis Salum maarufu “Salum Mbuzi” akizungumza wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi akizungumza
Muonekano wa eneo la mahafali
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Little Treasures Tilulindwa Sulus akizungumza katika mahafali hayo. 
Mwalimu mkuu wa shule hiyo,Paul Kiondo akizungumza wakati wa mahafali hayo
 
Awali wanafunzi wa shule ya Little Treasures wakiandamana kutoka Mwasele ambako ndiko shule hiyo ilianzia kabla ya kuhamia Bugayambelele kata ya Kizumbi. 
Wahitimu wa darasa la awali "Pre Unit" wakiingia ukumbini 
Wahitimu wa darasa la awali wakiingia ukumbini 
Wahitimu wa darasa la saba wakiingia ukumbini 
Wahitimu wa darasa la saba wakiingia ukumbini 
Wahitimu wa darasa la saba wakiingia wawili wawili ukumbini kwa madaha 
Wahitimu wa darasa la saba wakiingia ukumbini kwa kucheza 
Wanafunzi wakiimba wimbo wa taifa 
Mgeni rasmi akivalishwa skafu
Bendera rasmi ya shule ya Little Treasures Nursery & Primary School ikipandishwa kwa mara ya kwanza ambapo pia wakati wa mahafali hayo wimbo maalum wa shule hiyo ulizinduliwa.
Wahitimu wa darasa na saba wakiwa wamekaa na wazazi wao 
Wahitimu wa darasa la saba 
Wahitimu wa darasa la awali wakiwa eneo la tukio 
Wahitimu wa darasa la awali wakiwa katika eneo la tukio 
Wahitimu wa darasa la awali wakisalimia kwa kunyoosha mikono
Wageni waalikwa wakiwa katika mahafali hayo
Mwalimu Joyce Pius akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi wa shule hiyo 
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa katika mahafali hayo. 
Walimu na wanafunzi wakifungua shampeni... 
Meza kuu wakipata vinywaji baada ya shampeni kufunguliwa
Wanafunzi wa darasa la awali wakikata keki maalum kwa ajili yao 
Wahitimu wa darasa la saba wakikata keki maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao 
Wahitimu wa darasa la saba wakiendelea kukata keki 
Mhitimu wa darasa la saba akimlisha keki mgeni rasmi bwana Saleh Shaban Mohammed 
Mhitimu wa darasa la saba akimlisha keki Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic 
Mwenyekiti wa bodi ya shule Tilulindwa Sulus akimlisha keki mhitimu wa darasa la awali 
Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita akimlisha keki mtihitimu wa darasa la awali 
Wahitimu wa darasa la saba wakimlisha keki mwalimu wao wa darasa Alfred Gikaro 
Wanafunzi wa darasa la watoto "Baby Class" wakiimba wimbo 
Wanafunzi wa darasa la kati "Middle Class" wakiimba wimbo 
Wageni waalikwa wakiwa katika mahafali hayo 
Mahafali yanaendelea 
Wazazi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea 
Wanafunzi wa Hostel katika shule hiyo wakicheza 
Mahafali yanaendelea 
Mahafali yanaendelea 
Wazazi wakiwa katika eneo la mahafali 
Wanafunzi wa darasa la kwanza wakiimba 
Wanafunzi wakiwa katika mahafali hayo 
Tunafuatilia kinachoendelea...... 
Vijana wa Kimasai wakitoa burudani katika mahafali hayo. 
Akina mama wa Kisukuma wakiimba wimbo katika mahafali 
Wanafunzi wa darasa la Pili A wakiimba shairi 
Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic akielezea jinsi walivyoanzisha shule hiyo na wanafunzi hao waliohitimu darasa la saba mwaka huu 
Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic akicheza na wanafunzi wake 
Wanafunzi wakicheza
Mahafali yanaendelea 
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea 
Wanafunzi wakicheza wimbo wa Maria Rosa 
Wazazi wakifuarahia burudani 
Wanafunzi wahitimu wakicheza na kuimba 
Wahitimu wakicheza muziki 
Wanafunzi wa darasa la Sita wakicheza ngoma ya Kijaluo 
Meza kuu wakifuatilia burudani 
Wanafunzi wakicheza muziki 
Wageni waalikwa wakiwa eneo la tukio
MC Kifagio akitoa maelekezo kwa wazazi na walezi waliojitokeza kuchangia ujenzi wa jengo la bwalo katika shule hiyo 
Wageni waalikwa wakielekea meza kuu kutoa michango kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula kwa wanafunzi katika shule hiyo 
Wageni waalikwa wakiendelea kuchangia 
Wageni waalikwa wakishikana mikono na viongozi wakati wa kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula 
Wazazi wakiwaandaa watoto wao kupokea vyeti va kuhitimu darasa la awali 
Wazazi wakiwa na mtoto wao wakipiga picha ya kumbukumbu 
Zoezi la utoaji vyeti kwa wahitimu wa darasa la darasa la saba likiendelea
Picha ya pamoja,Mgeni rasmi,meza kuu na wahitimu wa darasa la saba.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »