NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewapongeza
wafanyakazi wa Mfuko huo, kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwatumikia
wateja, (wanachama) wa Mfuko.
Bw.
Mayingu ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwatunuku tuzo na
zawadi wafanyakazi waliofanya vizuri zaidi katika kipindi cha Wiki ya
Huduma kwa Wateja, iliyoanza Oktoba 2 na kumalizika Oktoba 6, 2017.
Wiki
hiyo ambayo huadhimishwa kila mwanzo wa wiki ya mwezi Oktoba kila
mwaka, hulenga kuwakumbusha wafanyakazi wajibu wao wa kuwahudumia wateja
kwa kuzingatia weledi wa utoaji huduma bora kwa mteja.
"Wakati
nikiwa Iringa nimepokea pongezi nyingi za Wanachama wetu, wakiwapongeza
nyinyi wafanyakazi kwa kuwahudumia vizuri, hongereni sana na niwaombe
muendele kutoa huduma bora kwa wateja wetu kwani huo ndio wajibu wetu."
Alisema Bw. Mayingu katika hafla hiyo iliyofanyika Oktoba 6, 2017 kwenye
ukumbi wa makao makuu ya PSPF, Jubilee Tower jijini Dar es Salaam.
Bw.
Mayingu aliwapongeza wafanyakazi wa Mfuko huo kote nchini, kwa kazi
nzuri na kuwaeleza kuwa kitendo cha wafanyakazi na maafisa wa Mfuko huo
kutoka maofisini na kuwafata wateja, (wanachama) majumbani kwao ili
kuzungumza nao na kuwahudumia kimesifiwa sana.
"Kaimu
Mkurugenzi Mkuu, alifuatana na baadhi yenu kwenda kule Kipunguni B. na
kukutana na mwanachama wetu, Bw. Kassim Mafanya, ambaye alikipongeza
kitedo kile na kusema hakutegemea maishani mwake yeye kama mstaafu
angetembelewa nyumbani kwake na PSPF, hili ni jambo jema." Alibainisha
Bw. Mayingu.
Wafanyakazi
waliopata tuzo ni Elizabeth Shayo, kutoka kitengo cha Huduma Kwa
Wateja, Makao Makuu, ambaye kupitia teknolojia, (mifumo), ni wateja
wenyewe ndio waliompendekeza kutokana na maoni yaliyopokelewa lakini
idadi ya watu aliowahudumia.
Mwingine
ni Bi.Valley Malinga, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), ambaye naye
alitunukiwa tuzo na kupewa zawadi kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya
wateja bila kuchoka.
Tuzo
hizo pia zimekwenda kwa walezi wa mikoa wa PSPF, kampuni mshirika ya
Ardhi Plan Limited na pia makampuni washirika yaliyoshirikiana na PSPF
kwenye wiki ya huduma kwa wateja, ambayo ni pamoja na Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya, (NHIF), Mabenki ya CRDB, NMB, TPB na Mwalimu Commercial
Bank (MCB).
Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiwahutubia wafanyakazi na wadau wa
Mfuko, wakati wa hafla ya kuwatunuku tuzo na kuwakabidhi zawadi
wafanyakazi "waliochomoza" kwa utoaji huduma bora zaidi katika kipindi
cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, 2017, iliyofikia kilele Oktoba 6, 2017.
Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Elizabeth Shayo.
Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo, Bi.Valley Malinga
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), Bi. Mwanjaa Sembe, (wapili kushoto), akiwa na maafisa waandamizi wa Mfuko huo.
Baadhi ya wafanyakzi wa PSPF
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akiwahutubia
wafanyakazi na wadau wa Mfuko, wakati wa hafla ya kuwatunuku tuzo na
kuwakabidhi zawadi wafanyakazi "waliochomoza" kwa utoaji huduma bora
zaidi katika kipindi cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, 2017, iliyofikia
kilele Oktoba 6, 2017.
Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Neema Muro, akihutubia wakati
wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi wa Mfuko huo mwshoni mwa Wiki ya Huduma kwa
Wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017
Mkurugenzi
wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Neema Muro, akihutubia wakati
wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi wa Mfuko huo mwshoni mwa Wiki ya Huduma kwa
Wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Oktoba 6, 2017
Meneja
wa Huduma kwa Wateja, Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Laila Maghimbi, (kulia),
na AfIsa Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. January Buretta, wakihakikisha kila kitu
kinakuwa sawa kwenye hafla hiyo
Baadhi ya wadau wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo
Sehemu
ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.
Sehemu
ya wafanyakazi waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya wadau wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo
Bw. Mayingu akimkabidhi tuzo Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF Bw. Delphin Richard, (kushoto)
Bw. Mayingu akimpatia zawadi Afisa Mipango Miji wa kampuni mshirika na PSPF, Ardhi Plan Limited, Bi. Anna Lukindo.
Mkurugenzi Mkuu na viongozi wengine wa Mfuko wakiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa wa tuzo
Picha ya pamoja na wadau
EmoticonEmoticon