Waziri wa Maliasili na
Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwa ameshika bidhaa za kampuni ya Ivori Iringa ambazo ni chocolate na pipi za maziwa alipotembelea banda la kampuni hiyo katika
maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia
katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya
kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa bi Amina Masenza walipotembelea banda la kampuni ya Ivori Iringa katika
maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia
katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya
kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiomuonyesha waziri wa Maliasili na
Utalii, Prof. Jumanne Maghembe baadhi ya bidhaa za kampuni ya Ivori Iringa katika
maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia
katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya
kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amezipongeza bidha zinazozalishwa na kampuni ya
Ivori Iringa (I.F.B) iliyopo mkoani Iringa kuwa ni dhaa zenyeubora unatakiwa
kwa afya ya mwanadamu hivyo kuwataka wananchi kuendelea kuzitumia ili kuvikuza
viwanda vyetu vya ndani vinavoyetengeneza bidhaa bora kama za kampuni hii.
Akizungumza wakati wa
kufungua maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini katika viwanja
vya kichangani mkoani Irirnga Prof.Maghembe amekuwa akitumia bidhaa za Ivori
mara kwa mara bado anazipenda kutokana na ubora wake.
“Hata akija mtu kutoka nje
ya nchi hawezi amini kama bidhaa kama hizi za Ivori zinatengezwa Iringa Tanzania
maana zimekuwa na ubora unastahili ndio maana leo kwenye maonyesho haya
nimetembelea kwenye banda hili na kukuta bidhaa mchanganyiko wa kampuni ya
Ivori Iringa (I.F.B)”alisema Prof. maghembe
Aidha Prof. maghembe
aliwaomba viongozi wa mkoa wa Iringa na watanzania kwa ujumla kuendelea
kuzitumia bidhaa hizo kwa kuzimia kwa lengo loa kuinua uchumi wa wazalendo hasa
hivi viwanda wa wananchi wazawa tuvikumbatie ili kuendelea kutoa ajira kwa
wananchi wengine.
“Nimeonja hizi chocolate za
kampuni ya Ivori Iringa kwa kweli kama zile ambazo huwa nazinunua nikiwa ulaya
au marekani jamani watanzania wenzangu tuendelee kutumia bidhaa bora
zinazotengenezwa na kampuni zetu za kizalendo” alisema prof. maghembe.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa
wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa kampuni ya Ivori Iringa imekuwa ikizalisha
bidhaa bora na zenye viwango vya kimataifa ndio maana zimekuwa zikipendwa na
watu wengi.
“Ukitembea karibia maeneo
yote hapa nchi Tanzania huwezi kuzikosa bidhaa za Ivori Iringa kutokana na
ubora wake hivyo wanasii tu waongeze wigo wa soko la bidhaa zao bila woga maana
zinaubora unaotakiwa” alisema Masenza
Lakini nikukumshe tu mnamo
tarehe 16 mwezi wa nne mwaka 2016 kampuni ya Ivori Iringa ilitoa angalizo kwa
watumiaji wa bidhaa zao kwa kuwa kumekuwa chocolate zinazofanana na chocolate
za kampuni hiyo.
Kama wewe ni mmoja kati ya
watu ambao umekua ukikutana na Chocolate inayotoka nje ya Nchi yenye nembo
inayofananishwa na Chocolate ya Ivori Iringa ukahisi labda wamebadilisha
muonekano wa nembo yao sasa Uongozi wa Kampuni ya IVORI IRINGA inayo majibu
yake kwenye hizi sentensi 5 na inabidi uzingatie pia unapoenda dukani kununua.
1-Kuhakikisha kila bidhaa
unayonunua ya IVORI ina Nembo Halisi ya IVORI yenye Herufi I mwanzoni na herufi
I mwishoni.
isomeke IVORI CHOCOLATE na
Sio IVORY CHOCOLATE
2-Bidhaa zetu zote
zinatengenezwa TANZANIA,Tunajivunia Uzalendo wetu na ndio maana bidhaa zetu
zote ni MADE IN TANZANIA .
3-Hakikisha kila Chocolate yetu unayoinunua ina Rangi ya
kahawia ndani ya pakiti yake ikiwa na Ladha tamu ya maziwa ikitegenezewa na
COCOA Halisi inayolimwa na Wakulima Nchini TANZANIA
4-Rangi ya kifungashio
chakeni ya Njano iliyochanganywa na Rangi ya Zambarau.
5-Gharama zetu Elekezi ni
Shilingi 1000 kwa Gram 40 na Shilingi 500 kwa Gram 20 na hatuna ujazo unaozid
gram 40.
Iwapo kuna utofauti wa
Bidhaa unayoiona na kuitilia shaka kampuni ya IVORI wanaomba sana uwasiliane
nao kwa sababu inabidi uwe Mjanja ili
Usidanganyike Kununua Bidhaa Feki,Nunua Bidhaa Orijino Za Ivori Iringa, Epuka
Kutapeliwa.
EmoticonEmoticon