Wataalam kutoka
, Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati
na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) na Mamlaka ua
Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) wakifuatilia
maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande (kulia)
pamoja na wataalam kutoka Uganda wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Nishati
na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo
pichani)
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi
Juliana Pallangyo (kushoto mbele) akieleza jambo katika kikao hicho.
|
Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akielezea hali ya utafiti wa mafuta na
gesi nchini.
Asteria Muhozya na
Greyson Mwase.
Timu ya wataalam
kutoka Uganda imewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na
wataalam wa Tanzania katika utafiti wa mafuta. Mbali na kubadilishana uzoefu
wataalam ha
Kabla ya kuanza kwa
ziara hiyo wataalam hao jana tarehe 2 Oktoba, 2017 wamefanya kikao kilichoongozwa na Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani na kuwashirikisha Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na wataalam
kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta
(PURA).
Akizungumza katika
kikao hicho, Dkt. Kalemani amesema
maandalizi hayo ni juhudi za Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli za kuhakikisha
kuwa rasilimali ya mafuta inagunduliwa na kuanza kuleta manufaa kwa wananchi,
ambapo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la Ujenzi wa Mradi ya Bomba la
Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima nchini Uganda
hadi Tanga nchini Tanzania tarehe 5 Agosti, 2017 alieleza kuwa wataalam
waliogundua mafuta katika Ziwa Abert nchini Uganda kushirikiana na wataalam wa
Tanzania katika utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na Eyasi nchini Tanzania.
Dkt. Kalemani amesema
baada ya Rais wa Uganda kukubali ombi hilo yalianza maandalizi kupitia vikao
mbalimbali ambapo hatua iliyofikiwa kwa sasa ni wataalam kukutana na
kubadilishana uzoefu kabla ya kuanza kwa shughuli za utafiti katika maziwa
husika.
Amesema wataalam
wataanza kwa kufanya ziara ya siku mbili katika Ziwa Eyasi Wembere mkoani Singida
ili kupata picha halisi kabla ya kuanza kwa majadiliano ya kubadilishana mawazo
ya namna bora ya utafiti katika maziwa husika.
“ Sisi kama Tanzania
tupo tayari kubadilishana uzoefu
na wataalam wa Uganda kwenye utafiti wa mafuta na kuanza kazi mara moja; hata hivyo pia tupo tayari kubadilishana nao uzoefu kwenye masuala ya gesi kwa kuwa tuna utaalam huo, lengo likiwa
ni kuimarisha sekta hizi za mafuta na gesi kwa nchi zote mbili,” amesema Dkt. Kalemani.
Ameongeza kuwa kwa
kuwa Tanzania ina uzoefu mkubwa kwenye utafiti wa gesi asilia, wapo tayari
kutuma wataalam nchini Uganda kushirikiana kwenye utafiti wa gesi nchini
Uganda.
Kwa upande wake Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda na
kiongozi wa ujumbe huo, Robert Kasande
amesema kuwa wapo tayari kubalishana uzoefu ambapo watalenga katika kuangalia
tafiti zilizowahi kufanyika nyuma, kutembelea maeneo husika na kuweka mikakati
ya namna bora ya kufanya utafiti kwa ubora wa hali ya juu kwa kushirikiana
na Tanzania.
EmoticonEmoticon