Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia
wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu
uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini
Dar es Salaam.
Wadau
wa sekta ya ujenzi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya
sekta hiyo kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la
Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto),
akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi),
Mhandisi Joseph Nyamhanga (kulia), katika warsha ya wadau wa sekta ya
ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi
(NCC), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mayunga Nkunya (kulia),
akifafanua jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa (kushoto), jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Dkt. Samson Mturi
akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya wadau wa
sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza hilo,
jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto),
akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Biashara Bw. Milton Lupa
(aliyesimama), kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakati
alipokagua mradi wa ujenzi wa nyumba za magomeni, jijini Dar es Salaam.
Mkadiriaji
Majenzi na Msanifu Majengo Neema Kifua (wa pili kulia), akitoa taarifa
kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za magomeni, alipotembelea
mradi huo leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka
wadau wa sekta ya ujenzi kuanza kuweka twakwimu takwimu zinazohusu
masuala ya ujenzi hapa nchini.
Akifungua
warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi
wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Prof. Mbarawa, amesisitiza umuhimu
wa sekta hiyo kuimarisha taarifa za aina, vifaa, viwango vinavyohitajika
kimataifa na gharama katika shughuli za ujenzi wa barabara, viwanja vya
ndege, nyumba na miundombinu mingine.
“Sekta
ya Ujenzi ina mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi
na kijamii hivyo uwepo wa taarifa mbalimbali unahitajika ili kurahisisha
uelewa wa wananchi wa kawaida katika masuala ya ujenzi na gharama
zake”, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha,
Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wadau wa sekta ya ujenzi kuwa
Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha sekta hiyo
inakidhi matarajio ya watanzania wengi kwa lengo la kuwajengea
miundombinu iliyo bora na imara.
Ameongeza
kuwa mapendekezo yatakayotolewa na wadau hao yatarahisisha utekelezaji
wa miundombiu mbalimbali ambayo italeta chachu kwa sekta nyingine
zikiwemo za kilimo, nishati, utalii, viwanda, madini na uendelezaji wa
biashara na nchi nyingine za kikanda.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi
Joseph Nyamhanga amesema ongezeko la miradi ya ujenzi imechangia
Serikali kutafuta wataaalm waliofanya tafiti kwa ajili ya uboreshaji wa
baraza hilo wataongeza tija na ufanisi wa sekta hii muhimu ya ujenzi kwa
wadau, wananchi na Serikali.
Naye, Mwenyekiti wa Baraza la NCC Prof.
Mayunga Nkunya amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa baraza lake
litasimamia michango yote itakayotolewa na wadau hao na kuahidi
kushughulikia changamoto zinazoikabili NCC ikiwemo za takwimu ili
kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kukua kwa kuwa ni sekta mtambuko.
Sekta
ya Ujenzi ni mojawapo ya sekta zinazokua kwa kasi hapa nchini na ina
mchango mkubwa kwa Pato la Taifa ambapo mwaka 2016 sekta hiyo ilichangia
asilimia 14 ya Pato la Taifa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
EmoticonEmoticon