Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,
Luhaga Mpina akikagua mfereji wa maji katika kiwanda cha Chemi Cotext
kilichopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam wakati wa ziara yake ya ukaguzi
wa mazingira.
NA;
EVELYN MKOKOI - DAR ES SALAAM
Akiendelea na ziara
yake ya ukaguzi na utekelezaji wa sheria ya Mazingira jijini Dar es
Saalaam, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina, ameagiza Baraza la taifa la Usimizi wa Mazingira NEMC
kwa kushirikiana na uongozi wa kiwanda cha kutengeneza unga wa Ngano
wa Azania, kupima kiwango cha ubora wa hewa inayoambatana na vumbi la
unga wa ngano linalotoka kiwandani hapo baada ya shughuli za uzalishaji
na kwenda kwenye mazingira na makazi ya watu kana vinakidhi viwango
vya kimazingira.
Mpina alisema kuwa baada
ya matokeo hayo yanayotegemewa kutoka baada ya wiki mbili, serikali
ndiyo itakuwa kwenye hatua ya kusema jambo kwa wananchi pamoja na kiwanda.
“Baada ya matokea
hayo sasa serikali inaweza kuwa na nafasi ya moja kwamoja kuchukua hatua
kwa mwenye kiwanda ikiwa ni pamoja na kukitoza faini kwa mujibu wa sheria,
na kama matokeo ya vumbi na kelele zitokazo kiwandani hapo yatakuwa
ndani ya kiwango, sasa hatua itakayofuata ni yakuangalia mahusiano kati
ya mwenye kiwanda na wakazi majirani wa eneo hilo. Alisema Mpina.”
Aidha Mpina aliongelea
kufaanyika kwa taratibu za kujua kama suala la kiwanda hicho kuwa karibu
na makazi ya watu , ni sahihi na kwa upande wa wananchi kuwa karibu
na kiwanda hususan kuwepo kwa nyumba kila baada ya hatua moja
nalo ni sahihi.
Awali katika muendelezo
wa ziara yake ya ufuatiliaji na utekelezaji wa sheria ya mazingira jijini
Dar es Salaaam, Naibu Waziri Mpina alikitembelea kiwanda cha Chemi
cotex kilichopo Mbezi Beach.
EmoticonEmoticon