KILOLO DC YASHIKA NAFASI YA TATU KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE YA NYANDA ZA JUU KUSINI

August 09, 2017
Mgeni rasmi katika kilele cha Maonyesho haya alikuwa waziri wa ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za Mitaa MHE. George B. Simbachawene akimkabidhi mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah tuzo ya mshindi wa tatu sambamba na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kilolo Aloyce Kwezi.Katikati DC wa kilolo Asia Abdallah , kushoto aliyeshika hati, Mkurugenzi Halmashauri ya Kilolo Aloyce Kwezi na mwishoni kwa Mkurugenzi ni Dkt. Mwingira Afisa Mifugo mkuu Wilaya na kulia tena huku ni Afisa Kilimo mkuu Wilaya ndgu. Kuziwa..

Na Fredy Mgunda, Mbeya

Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani iringa imeshika nafasi ya tatu katika maonyesho ya nane nane ambao huhusisha maswala ya kilimo yaliyofanyikia jijini mbeya kwa kanda ya nyanda za juu kusini na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali kutoka mikoa yote ya nyanda za juu kusini.

Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi ya kuwa washidi wa tatu wa maonyesho hayo ya nane nane  mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah aliwapongeza wananchi na viongozi wa wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika maonyesho hayo kwa kile walichokifanya na kuonyesha kuwa Kilolo Kilimo kinasaidia kuinua kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

"Mimi niwashukuru sana kwa zawadi waliyotupa wananchi na viongozi wa Wilaya ya Kilolo maana ushindani ulikuwa mkubwa mno hasa ukiangalia wilaya zote za nyanda za juu kusini zinasifika sana kwa Kilimo cha mazao mbalimbali na ufugaji hivyo haikuwa rahisi sana kufika hapa mwaka huu"alisema Abdallah

Abdallah alisema kuwa atakaa na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo Kupanga mikakati madhubuti ili mwakani waweze kushika nafasi ya kwanza na kuwa wilaya ya mfano huku nyanda za juu kusini hata Tanzania kwa ujumla.

"Sasa kazi imeanza na nitahakikisha kila kitu mwakani kitakuwa vizuri na tutafanya vizuri sana kwa kuwa halmashauri ya wilaya ya Kilolo ina maeneo mengi mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya Kilimo na ufugaji hivyo lazima tutatafuta njia mbada ya kuinua Kilimo cha wilaya ya Kilolo" alisema Abdallah

Aidha Abdallah alisema mikakati yake ni kuboresha pale walipokwama ili kupata matokeo chanya katika maonyesho yajayo.

"Mikakati iliyopo ni kwamba mwisho wa maonesho haya ndiyo mwanzo wa maonesho mengine, tumegundua vitu vilivyotufanya kuwa namba tatu ni pamoja na ubunifu, hivyo tutazidi kuwa wabunifu kwa maonesho yajayo ili tufikie ushindi mnono zaidi" alisema Abdallah


Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo Aloyce Kwezi alisema kuwa halmashauri inamikakati mingi ya kuboresha maeneo ya Kilimo kuwaomba wadau mbali mbali wanaotaka kuwekeza kwenye Kilimo wafike katika ofisi halmashauri ili kujadiliana namna ya uwezaji na maeneo wanayoweza kuwekeza.

"Halmashauri ya wilaya ya Kilolo ina maeneo mengi mazuri kwa ajili ya Kilimo ambayo bado hayafanyiwa Kilimo hivyo naomba wadau wenye nia ya kuwekeza kwenye Kilimo waje kuweza maana maeneo ni rafiki kwa Kilimo cha aina yoyote ile kutokana na hali ya hewa iliyopo huku" alisema Kwezi

Naye afisa mifugo mkuu wa wilaya ya kilolo Dkt. Mwingira aliupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo kwa jitihada za kuinua Kilimo na ufugaji kwa wananchi wa Wilaya hiyo na ndio sababu kubwa kupata mafanikio ya kushika nafasi ya tatu katika maonyesho ya nane nane.

"Mimi nampongeza sana Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi kwa ubunifu wao ambao umetusaidia kufika hapa hivyo naomba tuwape ushirikiano katika kukuza Kilimo cha Wilaya ya Kilolo "alisema Dr mwingira

Katika maonyesho hayo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa George Simbachawene na huku nafasi ya kwanza ilichukuliwa na halmashauri ya Mpanda na nafasi ya pili ilishikwa na Tunduru.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »