Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa akipokea Funguo ya Magari matatu yenye thamani ya Dola
za kimarekani 99,700 ambayo amekabidhiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Foton International kutoka China Bwana Zhao Xiano Kwa ajili
ya kusaidia shughuli zamaendeleo nchini Tanzania ,wanaoshuhudia kutoka
kushoto ni Meneja masoko wa kampuni ya Simba Motors Taanzania Bibi
Ifigenia Salazar na kutoka kulia ni Afisa masoko wa Foton International ,
Bwana Fan Liang .makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu
Magogoni Dar es salaam Agosti. 9. 2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akiangalia moja ya magari aliyo kabidhiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Foton International kutoka China Bwana Zhao Xiano Kwa
ajili ya kusaidia shughuli zamaendeleo nchini Tanzania. makabidhiano
hayo yamefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni Dar es salaam Agosti.
9. 2017
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amepokea msaada wa magari matatu yenye thamani ya Dola za Marekani
99,700 kutoka Kampuni ya Foton International Trade Co. Ltd ya nchini
China.
Amepokea msaada huo leo (Jumatano,
Agosti 9, 2017) jijini Dar es Salaam, ambapo amesema magari hayo
yatatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii nchini.
Magari hayo ni Sauvana SUV moja na Tunland Double cabin mbili.
“Nashukuru kwa msaada huu wa
magari uliotolewa na Kampuni ya Foton kwa Serikali yetu. Magari haya
yanaweza kutumika katika Hospitali za wilaya kwa ajili ya usambazaji wa
dawa na vifaa tiba pamoja na kutolea elimu mbalimbali kwa umma.”
Pia, Waziri Mkuu ameikaribisha
Kampuni hiyo kuja nchini kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha
kuunganisha magari. Amesema mbali na utulivu wa kisiasa uliopo Tanzania,
pia kuna sera na mazingira mazuri ya uwekezaji.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Zhao Xiao amesema wametoa msaada huo wa
magari kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo zinazofanywa na
Serikali ya Tanzania hususan maeneo ya vijijini.
Bw. Xiao amesema Kampuni ya Foton
inatengeneza magari 700,000 kwa mwaka, ambayo yanauzwa katika nchi 125
duniani. Amesea ifikapo mwaka 2020 wanatarajia kuongeza uzalishaji na
kufikia magari milioni 1.4 kwa mwaka.
Kuhusu suala la kuja kuwekeza
kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari nchini, Bw. Xiao amesema
wanampango wa kuwekeza nchini kwa kuwa kuna fursa nzuri za uwekezaji
na uhakika wa masoko katika nchi zingine za Afrika Mashariki.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, AGOSTI 9, 2017
EmoticonEmoticon