Na Mathias Canal, Lindi
Sekta ya Kilimo imetajwa kuwa bado ni muhimili wa
uchumi wa Tanzania kwa kuwa inatoa ajira kwa asilimia 65.5
ya Watanzania na kuchangia zaidi ya asilimia 100 ya chakula hapa nchi
katika miaka yenye mvua ya kutosha.
Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais,tawala za mikoa na
serikali za mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene
(MB) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya
wakulima - Nanenane, kwa mwaka huu wa 2017 katika viwanja vya maonesho ya
kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, tarehe 1/8/2017.
Alisema Kaulimbiu ya Nane Nane mwaka huu inasema “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za
Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati”. Kaulimbiu hii inahamasisha Wakulima, Wafugaji na
Wafugaji kuongeza uzalishaji na tija katika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Mhe Simbachawene alisema kuwa mwaka 2015, Sekta ya Kilimo ilichangia asilimia 29 ya
pato la Taifa, na mwaka 2016 ilichangia asilimia 29.1. Hivyo, ni dhahiri kuwa
mchango mkubwa katika pato la Taifa ulitokana na Sekta ya Kilimo ukifuatiwa na
Sekta nyingine za kiuchumi.
Alisema Kutokana na umuhimu huo, Serikali
inaeendelea kutekeleza mikakati ya kuongeza kasi ya kukuza kilimo, mifugo na
uvuvi ili kuchochea na kufikia uchumi wa viwanda sawasawa na Azma ya Serikali
ya Awamu ya Tano.
Alisema kuwa Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2016
uliongezeka kufikia kiwango cha utoshelevu wa asilimia 123 ikiwa ni zaidi ya
kiwango cha asilimia 120 cha mwaka 2015.
Hali hiyo, imechangiwa na ongezeko la asilimia 6.7
la uzalishaji wa mazao ya nafaka yakiwemo mahindi na mchele. Usalama wa chakula
pia unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mazao yasiyo nafaka kama vile mihogo,
viazi, ndizi na mazao ya jamii ya mikunde ambayo kwa ujumla kulikuwa na
ongezeko la uzalishaji wa asilimia 1.5
Pamoja na kiwango cha kuridhisha cha uzalishaji wa
mazao ya chakula, Mhe Simbachawene alisema kuwa hali mbaya ya hewa iliyojitokeza
mwisho wa mwaka 2016 na mwanzoni mwa mwaka 2017 ilisababisha kupanda kwa bei za
chakula katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Hata hivyo Katika kukabiliana na hali ya ukame
uliotokana na uhaba wa mvua za vuli na kuchelewa kuanza kwa mvua za masika
katika baadhi ya maeneo, hatua sitahiki zilichukuliwa.
Amezitaja Baadhi ya hatua hizo kuwa ni pamoja na kusambaza mbegu bora zinazokomaa
kwa muda mfupi, zikiwemo mahindi, mtama na mpunga huku vipando vikiwemo pingili
za mihogo na viazi vitamu vilisambazwa.
"Nchi yetu imebahatika kuwa na idadi kubwa ya
mifugo ikiwemo ngómbe, kondoo, mbuzi, kuku wa asili na kuku wa kisasa. Pamoja
na kuwa na idadi kubwa ya mifugo, viwango vya ulaji wa mazao ya mifugo hususani
nyama, maziwa na mayai bado viko chini. Katika mwaka 2016, mifugo inayouzwa
katika minada iliongezeka ukilinganisha na mwaka 2015 na hivyo kupata mapato
yanayotokana na ng’ombe shilingi trilioni 1.34, mbuzi na kondoo shilingi
trilioni 1.02" Alisema Mhe Simbachawene
Aliongeza kuwa Mapato yanayotokana na mauzo ya
ngozi yalifikia shilingi bilioni 34.7 kwa ngozi ya ngómbe, shilingi bilioni 6.2
kwa ngozi ya mbuzi na kondoo. Mapato yanayotokana na uzalishaji wa malisho
katika mashamba ya Serikali yalifikia shilingi bilioni 1.14. Aidha, mapato
yanayotokana na uzalishaji wa mbegu za malisho bora ya nyasi yalifikia shilingi milioni 55.8 na jamii ya
mikunde shilini milioni 11.
Waziri wa nchi
ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) akizungumza na Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakati wa uzinduzi wa maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya
maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.(Picha Zote na Mathias Canal)
Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakimsikiliza kwa makini Waziri wa nchi
ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya
maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Waziri wa nchi
ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB), Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb), na Mkuu wa mkoa wa
Mtwara Mhe Halima
Dendego wakitazama namna ya uzalishaji samaki katika banda la JKT wakati wa uzinduzi wa maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya
maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Waziri wa nchi
ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) akizungumza na Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakati wa uzinduzi wa maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya
maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb) akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tizeba wakati wa uzinduzi wa maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya
maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Mkuu wa mkoa wa
Mtwara Mhe Halima
Dendego akitoa salamu za mkoa wa Lindi na Mtwara wakati wa maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya
maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb) akisisitiza jambo alipozuru katika ukumbi wa JKT wakati wa uzinduzi wa maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya
maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Waziri wa nchi
ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (Mb) akionyesha moja ya mazao yanayozalishwa katika banda la JKT wakati wa maadhimisho
ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya
maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
EmoticonEmoticon