- Mkuu wa Wilaya Itilima –Benson Kilangi (kati kati ) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya NMB Itilima katika Mkoa wa Simiyu. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa NMB kanda ya Magharibi –Peter Madaha na Mbunge wa Itilima- Njalu Silanga wakishuhudia uzinduzi wa tawi hilo. Tawi hili ni miongoni mwa matawi mengine mawili yaliozinduliwa kwa pamoja katika kanda ya magharibi mwishoni mwa wiki.
- Mkuu wa Wilaya Igunga –John Mwaipopo (kati kati ) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya NMB Nkinga katika wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora wengine pichani ni Meneja wa NMB kanda ya Magharibi Leon Ngowi (wa kwanza kushoto) na Meneja wa NMB tawi la Nkinga Jasmina Tengia (kulia). Tawi hili ni miongoni mwa matawi mengine mawili yaliozinduliwa kwa pamoja katika kanda ya magharibi mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya
NMB imezidi kung’ara nchini huku ikifanikiwa kutanua mtandao wake kwa
kufungua matawi mapya matatu katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Simiyu.
Uzinduzi wa matawi hayo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo
kufunguliwa kwake kutaleta neema kwa wakazi wa maeneo hayo.
Mkoani
Kigoma benki hiyo ilizindua tawi jipya Wilaya ya Uvinza, Tabora
(Igunga) katika mji wa mashuhuri wa Nkinga na Simiyu Wilaya mpya ya
Itilima.
Awali
akizungumza katika uzinduzi wa tawi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza
Mkoani Kigoma, Mwanamvua Mrindoko, aliwataka wananchi wa wilaya hiyo
kutumia fursa ya benki hiyo ikiwemo kuhifadhi fedha zao na huduma za
kifedha ikiwemo mikopo nafuu inayotolewa na benki hiyo.
Alisema
hatua ya kuzinduliwa kwa tawi hilo la Benki la NMB sasa ni wazi wilaya
hiyo itajikwamua kiuchumi ikiwemo wananchi wake kujenga urafiki na benki
hiyo kwa kupata huduma bora za kifedha.
“Kuzinduliwa
kwa tawi hili jipya katika Wilaya yetu ya Uvinza sasa ni kielelezo
kwamba wananchi wataweza kujikwamua kiuchumi kwa kuwa na urafiki wa
karibu na benki ikiwemo kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa,”
alisema Mrindoko.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, John Mwaipopo,
akizinduwa tawi jipya katika mji wa Nkinga alisema ni kielelezo tosha
cha wilaya hiyo kupiga hatua kimaendeleo. Aidha akifafanua zaidi kwa
wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi huo, Mwaipopo alisema hatua hiyo
ni ishara nzuri na wananchi wataweza kutumia fursa kidekede zinazotolewa
na benki hiyo.
“Asanteni
NMB kwa kufika hapa Nkinga, awali wananchi walikuwa wakitembea umbali
mrefu hadi Igunga mjini kutafuta benki lakini sasa huduma za kifedha
zitapatikana hapa kupitia benki hii nzuri na bora kutokana na huduma
zake,” alisema Mwaipopo.
Naye
Meneja wa TRA Wilaya ya Nzega, Adolf Mtumbuka, akizungumza katika
uzinduzi huo, alisema tawi hilo litasaidia kukusanya mapato ya Serikali
ambapo awali wananchi wa Nkinga walilazimika kwenda makao makuu ya
wilaya.
“Ninapenda
sana kuishukuru Benki ya NMB sasa imekuja kufungua milango ya kiuchumi
katika eneo hili la Nkinga ambalo lipo Wilaya ya Igunga lakini pia lipo
jirani sana na Wilaya ya Nzega. Hivyo kuzinduliwa kwake kutasaidia
kukusanya mapato ya Serikali kupitia benki hii ambao pia hukusanya
mapato ya Serikali kwa niaba ya TRA,” alisema Mtumbuka.
Kutokana
na kuimarisha huko kwa mtandao wa benki hiyo Mkuu wa Wilaya ya Itilima
Mkoani Simiyu, Benson Kilangi, alisema kuzinduliwa kwa tawi hilo
kutachochea wananchi kuzalisha vizuri na fedha watakazopata watahifadhi
benki.
“Tunahitaji
kuweza ndani ya Wilaya ya Itilima ili wananchi wapate muda wa kutosha
katika shughuli za uzalishaji ili kuondokana na umaskini. Hivyo nawaomba
wananchi wa Itilima mtumie fursa hii ya Benki ya NMB kwa kisingizio
hamna mitaji au hajui mfanyaje.
--
______________________________ ______________________________ _______________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Web:- www.thehabari.com
EmoticonEmoticon