- Mkulima, Kidika Swai (mwenye suti ya kijivu) akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali (wa pili kushoto) pamoja na wakulima na wageni mbalimbali walipotembelea shamba hilo. Shamba hilo limepandwa kwa mbegu aina 11 bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA).
- Mkulima, Kidika Swai (mwenye suti ya kijivu) akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali (wa pili kushoto) pamoja na wakulima na wageni mbalimbali walipotembelea shamba hilo. Shamba hilo limepandwa kwa mbegu aina 11 bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA).
- Mratibu wa Mradi wa WEMA, na Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Ilonga, Dk. Justin Ringo (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali (wa pili kushoto) juu ya ubora wa mbegu chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA), katika moja ya shamba darasa la mkulima.
- Sehemu ya shamba la utafiti wa mahindi yenye sifa zifuatazo; kustahimili ukame na magonjwa, kukomaa mapema, zinazostawi ukanda wa chini na wa kati na zilizokaribia kuidhinishwa.
- Shamba darasa la mkulima, Kidika Swai lililotembelewa na washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani. Shamba hilo limepandwa kwa mbegu aina 11 bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA).
- Mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali akimenya moja ya hindi katika shamba darasa.
- Ofisa Mawasiliano wa jopo la watafiti wa Mradi wa WEMA Tanzania, Dk. Janet Kaya (kushoto mwenye kofia) akifafanua jambo kwa mgeni rasmi na viongozi wengine walipotembelea moja ya shamba mfano lililopandwa kwa mbegu chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA).
- Mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Makufwe (wa pili kulia) wakiangalia moja ya hindi kwenye shamba mfano lililohudumiwa na mbegu za mradi wa WEMA.
- Mkulima, Kidika Swai (mwenye suti ya kijivu) akitoa darasa kwa wakulima wenzake ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani.
Na Joachim Mushi, Handeni
WAKULIMA wa
Mradi wa utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame
(WEMA), wilayani Handeni wameiomba Serikali irekebishe sheria ya
uzalishaji wa mbegu ili kutanua wigo wa uzalishaji mbegu kupitia taasisi
za Serikali kama vile Jeshi la Kujenga Uchumi (JKT), Jeshi la Magereza
pamoja na zinginezo zilizopo.
Wakulima
hao wametoa ombi hilo jana kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakulima
Katika Kijiji cha Kabuku Ndani, kilichopo Wilaya ya Handeni mkoani
Tanga, kufuatia uwepo wa changamoto ya kutopatikana kwa uzalishaji wa
mbegu ya kutosha kulingana na mahitaji kama ile ya WE 2109 ambazo
zimeonekana kufanya vizuri zaidi maeneo ya Wilaya ya Handeni.
Akisoma
risala mbele ya mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mwakilishi wa Wakulima
hao, Costansia Msola alibainisha kuwa bei kubwa ya mbegu zinazozalishwa
na makampuni ya mbegu ulikuwa changamoto licha ya uwepo wa wadudu
waharibifu waliojitokeza kwenye mashamba ya wakulima na kukwamisha
matarajio ya uzalishaji.
Kwa
upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni,
aliyewakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali
aliwapongeza kikundi cha wakulima 22 waliokubali kushirikiana na
watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa
kushirikiana na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuendesha mradi wa
utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA)
ambao umeonesha mafanikio makubwa.
Aidha
aliwataka wakulima Wilayani Handeni kukubali mabadiliko na kuanza
kutumia mbegu hizo za kisasa zaidi ya aina 11 zilizoonesha mafanikio
makubwa katika utafiti. "...Huko nyuma tulikuwa tukitumia mbegu za asili
ambazo zilikuwa hazifanyi vizuri, naombeni sasa tutumie mbegu hizi bora
zilizofanyiwa utafiti na WEMA kwa kilimo bora," alisisitiza, Bw. John
Mahali akizungumza na wakulima.
Aliyaomba
makampuni ya uzalishaji mbegu kujitokeza na kufanya uzalishaji wa mbegu
bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame ili kuwasaidia wakulima
upatikanaji wake kwa wakulima.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Maendeleo ya Utafiti kutoka Wizara
ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Jackson Nkuba akimwakilisha Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Utafiti alisema Serikali ipo tayari kushirikiana na
makampuni yatakayojitokeza kuzalisha mbegu hizo bora kwa wakulima hivyo
kutoa rai kujitokeza kwa wingi. Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha
mkulima anafanya kilimo cha kisasa chenye tija apate mazao mazuri na
yakutosha ambayo yatamletea maendeleo. Alisema njia pekee ya kufanya
vizuri kwenye kilimo ni kuendesha tafiti mbalimbali na ndio sababu
Serikali kwa kushirikiana na mashirika anuai inaendelea kutoa fedha na
kufanya tafiti tofauti.
Hata
hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Makufwe
akizungumza aliiomba Serikali kujenga viwanda vya kusindika Mahindi na
mazao mengine yanayozalishwa na wakulima wilayani humo ili wakulima
wanufaike zaidi na mazao hayo, tofauti na kutegemea kuuza nje ya eneo
hilo. "Haiwezekani mahindi tulime sisi tuyauze Dar es Salaam na mikoa
mingine wayasindike (unga) na kuja kuuziwa tena sisi wenyewe wakati
mwingine kwa bei ya juu tofauti na tulivyo uza siye...," alisema Bw.
Mkufwe.
Mradi
wa utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame
(WEMA) ulianza mwaka 2009 ukiwa na lengo la kufanya utafiti shirikishi
wa mbegu bora chatara za mahindi zinazostahimili ukame kutokana na
mabadiliko ya hali ya hewa, ukiwa na mkulima mmoja tu lakini kwa sasa
una kundi la wakulima 22 ambao walihamasika na kujiunga pamoja
kushirikiana na watafiti.
- Baadhi ya wakulia wa Mradi wa utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA), wilayani Handeni wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani.
- Sehemu ya shamba la utafiti wa mahindi yenye sifa zifuatazo; kustahimili ukame na magonjwa, kukomaa mapema, zinazostawi ukanda wa chini na wa kati na zilizokaribia kuidhinishwa.
- Mtafiti na Mwenyekiti wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani, Wilaya ya Handeni, Bw. Temu (kulia aliyesimama) akiwasalimia washiriki wa maadhimisho hayo.
- Sehemu ya shamba la utafiti wa mahindi yenye sifa zifuatazo; kustahimili ukame na magonjwa, kukomaa mapema, zinazostawi ukanda wa chini na wa kati na zilizokaribia kuidhinishwa.
- Baadhi ya wakulima wakitembelea Shamba darasa la mkulima, Kidika Swai Shamba hilo limepandwa kwa mbegu aina 11 bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA).
- Sehemu ya shamba la utafiti wa mahindi yenye sifa zifuatazo; kustahimili ukame na magonjwa, kukomaa mapema, zinazostawi ukanda wa chini na wa kati na zilizokaribia kuidhinishwa.
EmoticonEmoticon