Sekta
ya utalii nchini imeendelea kukuza na kuongeza mapato ya serikali kwa kuchangia
zaidi ya asilimia 17 ya pato la taifa, huku ikitazamiwa kuongezeka katika mwaka
huu wa fedha.
Hayo yalisemwa Jana na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) Bwana Allan Kijazi
wakati akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA” kinachorushwa na Televisheni
ya Taifa (TBC1).
“Utalii unatoa mchango
mkubwa sana katika uchumi wa nchi hii, kwa sasa hivi unakisiwa kwamba
unachangia kama asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimia 25 ya fedha ya
kigeni,” alisema Bw. Kijazi. huku akisisitiza kuwa TANAPA watazidi kulinda na
kuendeleza hifadhi zilizopo nchini ili zizidi kuongeza pato la taifa kwa
maendeleo ya watanzania wote.
Mkurugenzi huyo wa
TANAPA alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 TANAPA ilichangia kiasi cha
billion 27 kwenda Mfuko wa Taifa wa serikali na matarajio yao katika kuchangia
mfuko wa fedha wa Taifa kwa mwaka huu wa
fedha 2017/2018 ni bilioni 33.4 hii ni kwa sababu ya kuongezeka kwa Watalii
kutoka nje ya nchi.
Aliongeza kuwa Tanzania
ina vivutio vingi kama vile Mito, Mabonde, Milima, lakini hifadhi za Taifa kama
Vile Ngorongoro, Serengeti, Gombe, Ruaha ndizo zinazoongoza kwa kuchangia pato
la taifa kwa zaidi ya asilimia 80 ikilinganishwa na vivutio vingine.
Bwana Kijazi aliongeza
kwa kusema kuwa, utalii nchini umekuwa ukikuunaongezeka kila mwaka ambapo kwa
takimwu walizo nazo zinaonesha kuwa, ongezeko la watalii kwa miaka mitano iliyopita
limekuwa lilkiongezeka kwa asilimia 4 hadi 7 kila mwaka.
Kuongeza kwa watalii
hasa katika hifadhi za Taifa kunatokana na TANAPA kujitangaza zaidi katika nchi
mbalimbali duniani kupitia Mitandao ya kijamii, Makampuni binafsi ndani na nje
ya nchi, Balozi za Tanzania katika mataifa ya Nje, Vilabu mbalimbali vya Ulaya
na Amerika pamoja Vyombo vya Habari vya kimataifa kama vile CNN na BBC.
Mkurugenzi Kijazi
alisema kuwa, Mataifa yanayoongoza kutembelea hifadhi za taifa ni pamoja na
Marekani, Ujerumani, Uingereza, Italia, Ufaransa, pamoja na Hispania huku akitaja
kuwa vivutio vya utalii vilivyopo Nchini hasa hifadhi ni vya kipekee, mazingira mazuri,
hali ya hewa pamoja na amani na utulivu uliopo nchini ndiyo sababu zinazowavutia watalii kuongezeka kila mwaka.
Pamoja na kukua na
kuongezeka kwa utalii nchini kunakopelekea kuongeza la Taifa, Mkurugenzi Kijazi
alisema kuwa, utalii wa ndani bado ni changamoto kwani watalii wengi wanatoka
nje ya Nchi huku wazawa wakishindwa kuzuru maeneo mbalimbali ya utalii ili
kujionea fahari ya nchi yao hivyo ametoa wito kwa Watanzania kutembelea vivutio
hivyo ili kukuza na kuongeza pato la Taifa.
Hivi karibuni Mtandao
wa SafariBookings.com unaojihusisha na masuala ya ukuzaji wa safari za kitalii
barani Afrika uliitaja Tanzania kama kivutio kizuri cha safari za
watalii barani humu.
EmoticonEmoticon