TSN Group Tanzania na MIMOSA CONCIERGE wasaini Mkataba leo Dar es salam

July 18, 2017

TSN Group Tanzania, katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake hapa nchini, imeingia mkataba na MIMOSA CONCIERGE inayotoa MIMOSA Black Card ambayo ni kadi maalum kwa wateja wanaofika kupatiwa huduma kupitia kadi hizo.
Meneja Masoko wa TSN, Jahu M. Kessy Pamoja na  Mkurugenzi Msiaidizi wa MIMOSA, Leonce Mongi wakati wa kusaini mkataba na MIMOSA CONCIERGE inayotoa MIMOSA Black Card ambayo ni kadi maalum kwa wateja wanaofika kupatiwa huduma kupitia kadi hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba huo na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, leo Meneja Masoko wa TSN alisema, Jahu M. Kessy amesema TSN imelenga kuongeza tija katika kutoa huduma zake.

“Tunarahisisha na kuboresha huduma zetu kuwa bora na za kisasa. Pengine huduma hii itapanua wigo wa wateja wetu watumiao Black Cards kwa Dar es salaam lakini kwa Mwanza TSN Hypermarket inakuwa kampuni ya kwanza kupokea na kukubali malipo kupitia Black card ya Mimosa. Hatua ambayo ni kubwa kuchukuliwa na TSN katika kuwajali wateja wake.”

“Sasa ukifanya malipo kupitia kadi ya Mimosa kwenye supermarket zetu na Petrol station unajiweka katika nafasi ya kushinda punguzo la zaidi ya asilimia 5 pamoja na kuponi ya zawadi wa kwateja watakao tumia kiasi cha shillingi laki moja kwa manunuzi ya mara moja,” alisema Jahu.
Akieleza zaidi juu ya huduma na faida wazipatazo wateja watumiayo kadi hizo, Mkurugenzi Msiaidizi wa MIMOSA, Leonce Mongi alisema kupitia kadi hii Mteja wa TSN hatapata tu punguzo la bei kutoka TSN pekee lakini pia atapata offer mbalimbali zitokanazo na kadi hiyo kupitia discount partners wengine ambao ni zaidi ya watoa huduma 71 Nchi Nzima. 

Jahu alisema TSN inajiimarisha katika kutoa huduma zake kwa wateja, kuwasikiliza na kuwasaidia, hivyo basi kuona umuhimu wa kuwapatia wateja wake wenye MIMISA black card nafasi ya kufanya malipo yao kwa uhuru na furaha.

Alisema,”hatua hii inafuatia hatua nyinginezo nyingi tulizochukua kuhakikisha wateja wa TSN wanafurahia huduma zetu, ikiwemo malipo kutupitia miamala ya simu, bank cheques, malipo ya dola na sasa pia kupitia Mimosa Black Card.
Leonce alisema kupitia kadi hii TSN itakuwa ikipokea malipo na kuongezaa tija kwa mteja, lengo ni kuhakikisha mteja mwenye kadi ya Mimosa hashindwi kufanya malipo yake akiwepo katika vionga vyao, na pia kufurahia ofa na punguzo mbalimbali zipatikanazo na mtangamano huu.

 “Teknolojia imeendelea kuwa kitovu cha maendeleo ya jamii yetu kwa kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. Kukua kwa teknolojia katika nyanja mbalimbali za kiuchumi kisiasa na kijamii kumeendelea kuleta matokeo chanya siku hadi siku. Sambamba na kurahisishwa kwa utendaji kazi lakini pia upokeaji wa huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wa kawaida kumerahisishwa.” Alisema Jahu.
Katika kutambua fursa hiyo, TSN itaendelea kujidhatiti katika kuhakikisha kuwa huduma kwa wananchi zinaenda sambamba na mabadiliko hayo ya teknolojia.
Leonce aliipongeza TSN kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inaweka urahisi kwa wateja wake na hiyo imekuwa ni chachu kubwa katika kurahisisha utoaji huduma kwa wateja wao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »