Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Mwandishi wa Habari wa kituo
cha Radio cha Efm kinachopatikana katika masafa ya 93.7 katika jiji
la Dar es Saalam alipokuwa akimuuliza maswali kuhusu uchafuuzi wa mazingira utokanao na
uchimbaji wa mchanga katika eneo la Boko.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na vyombo vya habari baada
ya kukamilika kwa zoezi la kukagua mto Nyakasangwe, uliopo katika kata
ya Bunju ulioharibiwa vibaya na uchimbaji wa mchanga.
Katika picha eneo la mto Nyakasangwe lililopo kaika
kata ya Bunju linavyoonekana kuharibika vibaya kutokana na uchimbaji
wa mchanga , na kupelekea makazi ya wananchi kuwa hatarini.
Eneo la mto Nyakasangwe lililogeuzwa kuwa Dampo na
wakazi wa eneo hilo lililopo katika kata ya Bunju. (Picha na Evelyn
Mkokoi)
NA; EVELYN MKOKOI
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Luhaga Mpina ,amesitisha uchimbaji na uchotaji wa mchanga
kiholela katika maeneo yasiyo rasmi.
Pia ametoa siku 30 kwa Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kubaini
na kutenga maeneo ya uchimbaji ya mchanga ambayo yapo ndani ya manispaa
zao yatakayo ruhusiwa kwa zoezi hilo kisheria.
Akitoa agizo hilo Dar es Salaan leo,wakati wa ziara
ya kutembelea Mto Nyakasangwe uliopo maeneo ya Boko Kata ya Bunju alisema
kama kuna maeneo ambayo wananchi wanaweza kufika Kwa urahisi, manispaa
zinapaswa kuyatembelea maeneo hayo na kuyabaini kama kunauwezekano wakuchimba
mchanga.
Alisema ndani ya mwezi mmoja manispaa hizo zinatakiwa kuandaa utaratibu mfupi
wa kutenga maeneo hayo ikiwemo utoaji wa vibali kutoka Wizara ya Nishati
na Madini,Halmashauri pamoja na Nemc.
“Halmashauri zote zilizo na eneo ambalo linaweza
kuruhusiwa kuchota mchanga hakikisheni mnatembelea maeneo hayo na kufata
taratibu zote za utoaji wa vibali ambapo maeneo mengine yawe ya uchotaji
wa mchanga,”alisisitiza Mpina
Alisema watafanya Operasheni ya usiku na mchana kuhakikisha
watu watakaoendelea kuchimba mchanga na kuchota mchanga sehemu ambazo
haziruhusiwi watachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kutozwa faini zilizopo
kisheria na kufikishwa mahakamani.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunju Bw. Kateni
Nassor Msangi alimshukuru Mpina kwa kufanya ziara katika eneo hilo na
kuiomba serikali kufanya utaratibu wa kujengea mawe katika kuta za kingo
yam to huo ambao umeharibika vibaya, ili kuweza kunusuru mazingira ya
mto huo kuharibika pamoja na kunusuru makazi yao.
EmoticonEmoticon