Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori
akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) katika Ofisi za
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori
akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzungumza
katika kikao kazi na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi
katika Manispaa hiyo leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na
viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika Manispaa
hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa
umma leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Chama cha TALGWU, Bw. Ibrahim Zambi
akiwasilisha hoja mbalimbali zinazowahusu watumishi wa umma wakati
wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao
kazi na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.
Askari Msaidizi wa Manispaa ya Ubungo, Bw. Germini
Massawe akiwasilisha malalamiko kuhusu kada yake wakati wa ziara
ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na
watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi-Idara ya Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi,
Bi. Loyce Lugoye akifafanua jambo kuhusiana na masuala ya kiutumishi
wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na
watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kilichofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.
Waajiri nchini wametakiwa kuzingatia mgawanyo sahihi wa Rasilimaliwatu
katika Utumishi wa Umma ili kuwa na utendaji bora na wenye matokeo katika
utumishi wa umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na
Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es
Salaam.
Mhe. Kairuki amesema mwajiri anapoomba kibali cha kuajiri watumishi ni vema
akazingatia mahitaji kulingana na majukumu yaliyopo ili kuondoa ziada ya
watumishi wa umma wasio na kazi kuendana na fani walizosomea kwa lengo
la kuwa na utendaji mzuri.
“Ni vizuri sana wakati tunaomba vibali vya kuajiri watumishi wa umma
tukazingatia mgawanyo sahihi wa rasilimaliwatu katika maeneo yetu kulingana
na majukumu ya watumishi tunaowahitaji badala ya kuomba watumishi wengi
ambao wanasababisha kuwa na ziada ambayo haitumika ipasavyo” Mhe.
Kairuki amesema.
Waziri Kairuki amesema katika vibali 10,184 vilivyotolewa hivi karibuni na Ofisi
ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa Mamlaka
za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali, pamoja na
Taasisi na Mashirika ya Umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa
umma waliobainika kughushi vyeti vya elimu, Halmashauri ya Manisapaa ya
Ubungo imetengewa jumla ya nafasi 140.
Aidha, ameongeza kuwa, Halmashauri hiyo imetengewa jumla ya nafasi za
ajira mpya 397 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hivyo zitendewe haki kwa
kuhakikisha watumishi watakaoajiriwa wanafanya kazi kwa mujibu wa mpango
uliopo.
Mhe. Kairuki yuko katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama kwa
lengo la kukutana na watumishi wa umma na kusikiliza malalamiko, ushauri na
changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia
kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo
yaliyopangwa na Serikali.
EmoticonEmoticon