“MILIONI 10 ZINAHITAJIKA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA MBIO ZA MAGARI MKOANI TANGA “

June 15, 2017
CHAMA cha mbio za magari mkoani Tanga (Tanga Motors Sports Club (TMSC) kimesema kinahitaji milioni 10 kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Tanga Rally 2017 yanayo tarajiwa kufanyika  Julai 8 mpaka 9 mwaka huu mjini hapa.

Akizungumza jana, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Awadhi Bafadhili
  alisema mashindano hayo msimu huu yatashirikisha washiriki kutoka nchini mbalimbali ikiwemo Kenya na Tanzania ili kuweza kumpata bingwa

Alisema hivi sasa wanachokifanya ni kuangalia kama kutakuwa na

uwezekano wa kubadilisha njia kutoka Pongwe na Muheza kutokana na kuharibiwa vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha na hivyo inaweza kuwa kikwazo cha kushindwa kufikia malengo yao.

Makamu Mwenyekiti huyo alisema  katika mashindano hayo msimu huu
  kunatazamiwa kuwa na madereva maarufu ambao wanafanya vizuri mkoani Tanga, Ally Kiraka,Ashu Barbosa,Utu Nizimal,Ottu Nirmal,Twalib Khatibu,Anthony John, Naeel Asher na Said Baghzah ambao ni tishio kwa mchezo huo.

Alisema licha ya madereva hao lakini wengine ambao wataungana nao ni
  kutoka mikoa ya Arusha,Moshi,Dar,Iringa na Morogoro ambao ni Mzee Gerald Miller,Ahmed Huwell,Sameer Nahdi, Dharam Pandya,Sunny Birdi,Jamil Khan na Isaac Taylor ambao uwepo wao umepelekea mashindano hayo kuonekana yatakuwa na ushindani mkubwa.

Aidha pia alisema mpaka sasa tayari wafadhili watatu wameonyesha nia
  ya kusapoti mashindano hayo ambayo ni Kiwanda cha Unga cha Pembe na Mkwawa Power Drinking water cha Mkoani Iringa na Mkwabi Super Market.

Akizungumzia changamoto ambazo wanakumbana nazo wakati wa mashindano
  hayo alisema mojawapo ni kitendo cha madereva wa pikipiki na baiskeli maarufu kama bodaboda kukatiza barabarani wakati wa mashindano hayobila taarifa jambo ambalo ni hatari.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »