Bi Lailatu Jethwa Meneja Mauzo
Samsung (Kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari stika mbili
zinazolenga kutokomeza bidhaa feki nchini katika mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika jijini Dar es Salaam Jana. Katikati ni, Meneja wa
Samsung Nchini Bw Rayton Kwembe, akifatiwa na meneja bidhaa wa Samsung
Bw Elias Mushi, Meneja wa Phyramid consumers Karen Babu na Lulu Chiza
Mkurugenzi wa masoko Phyramid consumers.
Bi Lailatu Jethwa Meneja Mauzo
Samsung (Kushoto) akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni
yao mpya ya Nunua sajili na Ushinde inayolenga kutokomeza bidhaa feki
nchini katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es
Salaam Jana. Katikati ni, Meneja wa Samsung Nchini Bw Rayton Kwembe,
akifatiwa na meneja bidhaa wa Samsung Bw Elias Mushi na Meneja wa
Phyramid consumers Karen Babu
Bi Lailatu Jethwa Meneja Mauzo
Samsung (Kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari bidhaa
zinazohusishwa katika kampeni yao mpya ya ‘Nunua sajili na Ushinde’
inayolenga kutokomeza bidhaa feki nchini katika mkutano na waandishi wa
habari uliofanyika jijini Dar es Salaam Jana. Kulia ni, Meneja wa
Samsung Nchini Bw Rayton Kwembe.
…………………………..
Samsung wazindua stika mbili za kupambana na bidhaa feki
Samsung wazindua stika mbili kwa utambuzi wa bidhaa Halisi
Samsung waungana na Pyramid consumers kukuza soko Tanzania
Dar es salaam, June 2017. Samsung
Tanzania wameanzisha mfumo wa kuweka stika mbili katika bidhaa zao kwa
ajili ya utambuzi wa bidhaa zao halisi pamoja na kupambana na bidhaa
feki nchini. Sambamba na mkakati huo Samsung piawameanzisha Kampeni ya
‘Nunua Sajili na Ushinde’. Kampenihiyo ya mwezi mzima inayolenga
kutokomeza bidhaa feki nchini itaanza tarehe 16 ya mwezi juni katika
mikoa yote ya Tanzania, na itaambatana na promosheni kabambe
inayotarajiwa kuwazawadia mamilioni ya watanzania watakao nunua bidhaa
halisi za Samsungkama vile TV, Friji, Microwave, mashine ya kufulia
pamoja na Viyoyozi.
“Ukizingatia bidhaa feki zina
hatarisha afya za watumiaji, mahitaji ya bidhaa bora na halisi
yanaongezeka kwa kasi kila kukicha. Samsung tumeendelea kufanya jitihada
zaidi katika kukidhi matakwa ya wateja wetu ulimwenguni pamoja na
Tanzania kwa ujumla. Samsung Tanzania inaamini kwamba kampeni ya ‘Nunua,
Sajili, Na Ushinde’ itaongeza uzoefu mpya na uelewa kwa wateja wetu wa
dar es salaam na mikoani pia juu ya utambuzi wa bidhaa feki zisizo kuwa
za Samsung” alisema Meneja Bidhaa kutoka Samsung, Bw. Elias Mushi.
Akiongeleakuhusumkakati huo mpya
Bw Mushi alisema ‘tumeongeza alama mpya kwenye bidhaa zetu ambazo ni
stika mbili zitakazo wasaidia wateja kutambua bidhaa feki sokoni, Bidhaa
za Samsung zitakuwa na stika mbili, stika msambazaji na stika
inayotambulisha bidhaa halisi ya Samsung. Kampeni ya ‘Nunua Sajili na
Ushinde’ itakua ni kiunganishi cha kupeleka elimu kwa wateja wetu ambayo
itawapa taarifa za bidhaa zetu zinazoenda sambamba na mahitaji ya
matumizi yao.
Pamoja na kampeni hiyo kabambe
Samsung wataendesha bahati nasibu ambayo washindi watajinyakulia zawadi
kila siku kwa muda wa mwezi mmoja. Wateja wa Samsung watafaidika na
mpango huu kwa kusajili namba za bidhaa zao mara tu wanaponunua bidhaa
hiyo. Hii itafanyika kwa kutuma namba ya bidhaa kwenda namba 0798222333.
Wateja watapata meseji ya uthibitisho wa bidhaa halisi ya Samsung papo
hapo. Kwa kufanya hivo Mteja atakuwa amejiunga moja kwa moja kwenye droo
ambayo itamwezesha kuwa mshindi wa bidhaa bora za Samsung zinakuja na
waranti ya miezi 12.
Kusherehekea uzinduzi huo wa Nunua
Sajili na Ushinde pamoja na kusambaza elimu juu ya stika hizo mbili kwa
watanzania Samsung inaendesha kampeni ya uhamasishaji nchi nzima kwa
kipindi cha mwez mmoja.
Kwa kupitia mkutano wa vyombo vya
habari uliofanyika makao makuu ya Samsung. Samsung wametangaza kuingia
ubia wa usambazaji na kampuni ya Tanzania Pyramid Consurmers ltd.
Makubaliano yamehusisha usambazaji wa bidhaa mpya na za kisasa za
kieletroniki za Samsung. Makubaliano hayo yatapelekea makampuni hayo
mawili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa bora na halisi za Samsung ndani
ya Tanzania.
Bidhaa za Samsung ambazo
zinasambazwa mpaka sasa na Tanzania Pyramid Consumers ltd, ni pamoja na
tv, friji, viyoyozi, mashine za kufulia pamoja na microwave.
Akifafanua kuhusu makubaliano hayo
Bw Mushi alisema “tunafuraha kuungana na Tanzania pyramid consumers ltd
kwenye usambazaj wa bidhaa zetu. Tupo mbioni kutambulisha bidhaa zetu
mpya na pia tumejipanga kuongeza uwepo wetu nchi nzima kwa ajili ya
kurahisisha upatikanaji wa bidhaa bora na halisi za Samsung nchini”
akaongeza kuwa “lengo letu ni kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wetu
kila Nyanja pamoja na kutanua wigo mpana wa mauzo pamoja na kuwafika
wateja wetu maana wao ndo nguzo ya mafanikio yetu. Muungano wetu na
Pyramid Consurmers umetufanya tuwafikie wateja wetu kwa urahisi, kwa
haraka na kwa kuwapa mahitaji sahihi kwa kile wanachohitaji”
Karen Babu Meneja wa Pyramids
consumers aliongezea kuwa “ Samsung ni kampuni kubwa inayozidi
kujitanua na yenye ubunifu wa hali ya juu kwenye bidhaa zake hivyo
tunajivunia kutumia uzoefu wetu na ujuzi tulionao kufanikisha malengo
haya yote kwa pamoja. Pia tunajivunia kushirikiana na Samsung kwa pamoja
tutafanikisha kufikia soko la Tanzania kwa kiwango cha juu”
KUHUSU KAMPUNI YA SAMSUNG
Samsung Electronics ni kampunia ya
vifaa ya teknolojia iliyoa ajiri zaidi ya wafanyakazi 236,000 kwenye
nchi 79 ulimwenguni. Samsung imeongeza ukuaji mkubwa wa teknolojia
kwenye bidhaa kama TV, CAMERA, VIYOYOZI, SIMU, FRIJI, VICHAPISHAJI na
kadhalika, ilikufikia mahitaji ya watumiaji kulingana na ukuaji wa
teknolojia. Kufahamu zaidi tembelea tovuti ya www.samsung.com. au www.facebook.com/SamsungElectronicsTanzaniana akaunti ya istagram: Samsung Tanzania
EmoticonEmoticon