Jovina Bujulu-MAELEZO.
Baadhi
ya wasomi wameonyesha kuridhishwa na kuunga mkono hatua ya Rais John
Magufuli kuagiza wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria baada ya
kupokea ripoti ya pili ya Kamati ya Wachumi na Wanasheria aliyoiunda kwa
ajili ya kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya
nchi.
Akiongea
na Idara ya Habari (Maelezo) Dk Benson Bana ambaye ni Mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam alisema kitendo kilichofanywa na Rais Magufuli
kimewafungua macho viongozi wengi wa Afrika na dunia na kitakuwa ni
mfano wa kuigwa kwa Serikali nyingi za Afrika na dunia kwa ujumla
“Ningefurahi
kama tungetenga siku maalumu kuandamana kwa nia ya kuunga mkono nia
njema ya Rais ya kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi hii hazitumiwi
hovyo hovyo” amesema Dk Bana.
Aliongeza
kusema kuwa kitendo cha kutafuta ukweli katika makinikia na biashara ya
madini na kuweka wazi taarifa hiyo kwa umma na kusema wahusika wa
sakata hilo wachukuliwe hatua za kisheria kimeonyesha uzalendo wa dhati
kwa nchi yake.
Aidha
aliunga mkono kitendo cha Rais kukubali kufanyia kazi mapendekezo yote
21 yaliyotolewa na Tume ya Uchunguzi, kwani yataweka wazi mwenendo mzima
wa biashara ya madini na kuziba mianya ya wizi wa madini.
Dk.
Bana alimpongeza pia Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba kwa
kuchukua uamuzi wa haraka wa kuwazuia kusafiri nje ya nchi watuhumiwa wa
sakata hilo.
Alisema
wale wote waliotajwa kuhusika na suala hilo kukaa nje ya utumishi wa
umma kwa muda wakati uchunguzi dhidi yao ukiendelea na endapo
watabainika kuwa hawana hatia warudishwe kazini na ikibainika kuwa
walihusika wachukuliwe hatua stahiki.
Alitoa
wito kwa Watanzania kuuunga mkono nia njema ya Rais Magufuli kwa
sababu hatua hiyo ni harakati za kuweka sawa uchumi wa nchi ili
kuboresha maisha ya Watanzania.
EmoticonEmoticon