Mkuu
wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Sophia Njema
akizungumza na Jonas Hans Atile (kushoto) ambaye amejitokeza kuchangia
Damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Leo.
Mkurugenzi
wa Huduma za Tiba Shirikishi Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Dk. Praxeda Ogweyo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
maadhimisho ya Siku ya Kuchangia Damu Duniani. Pia Dk. Ogweyo amewataka
Watanzania wajitokeze kwa wingi kuchangia damu.
Mmoja wa Wananchi akishiriki katika maadhimisho ya Siku ya Uchangiaji Damu duniani Leo katika hospitali hiyo.
Baadhi ya wananchi wakisubiri kuchangia damu Leo katika jengo la Maabara kuu, hospitali ya Taifa Muhimbili
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza kuchangia damu katika Hospitali ya Muhimbili wakiendelea na shughuli ya utoaji damu Leo.
……………………………….
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imeshiriki katika madhimisho ya Siku ya
Kuchangia Damu duniani kwa kuendesha shughuli ya utoaji damu kwa watu
mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya huduma hiyo kwa wagonjwa wenye
uhitaji.
Shughuli
hiyo inaendelea katika hospitali hiyo kwenye Jengo la Maabara kuu
ambako watu wamekusanyika kwa ajili ya kuchangia damu. Mmoja wa viongozi
walishriki katika maadhimisho hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini
Dar es Salaam, Mheshimiwa Sophia Mjema pamoja na Watanzania mbalimbali.
Akizungumza
katika shughuli hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewataka
Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya
wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo wakiwamo kinamama na watoto wadogo.
“Nawapongeza
wote walifika leo hapa Hospitali ya Muhimbili kuchangia damu, ni jambo
la muhimu mmefanya kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa,” amesema
Mheshimiwa Mjema.
Naye
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa hospitali hiyo, Dk Praxeda
Ogweyo amewataka wananchi,mashirika ya umma na yasiyo ya kiserikali,
shule, vyuo mbalimbali na taasisi za dini kujitokeza kuchangia damu
hospitali hapo.
Dk
Ogweyo amesema kuwa Muhimbili inahitaji wastani wa chupa za damu 100
hadi 120 kwa siku na kwamba damu inayokusanywa ni kati ya chupa 50 hadi
60 na upungufu wa damu ni chupa 60 hadi hadi 70, hivyo damu inahitajika
zaidi.
“Kutokana
na hali hii, naomba rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuokoa
maisha ya wagonjwa. Hospitali imejipanga kupitia kitengo chake cha
uchangiaji damu kilichopo maabara kuu hivyo karibuni mchangie damu,”
amesema Dk Ogweyo.
PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
EmoticonEmoticon