Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr.Donalth
Ulomi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza
hati iliyopewa kampuni hiyona ambayo inaiwezesha Kampuni kumilikiwa na Umma wa
watanzania.
Akiongea na Wanahabari Dr. Ulomi amesema kwamba Kuanzia
Sasa Kampuni ya Maxcom Africa itatambulika kwa Jina la Maxcom Africa Public
Limited Company (Maxcom Africa PLC) . Kampuni hii maarufu kwa jina la Maxmalipo ni Moja ya
Kampuni zilizoanzishwa na kuendeshwa na wazawa watanzania ambayo imeifikia
hatua za Mwisho katika mchakato wa kuanza kuuza hisa zake kwenye soko la
hisa. Dr. Olumi amewaambia wanahabari kwamba wanasubiri kibali cha
wasimamizi wa Soko la Hisa ili waweze Kuorodhesha Kampuni yao katika Soko hilo
Mjumbe
wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr. Donalth Ulomi (kulia ) akikata utepe wa
kuzindua rasmi Jina Lipya la Kampuni ya Maxcom Africa PLC anayeshuhudia
ni Mkurungezi wa Uendeshaji wa Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika
hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa PLC Kijitonyama
Jijini Dar Es Salaam.
Mjumbe
wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr,Donalth Ulomi (kulia ) akionesha nembo
ya jina jipya Maxcom Africa PLC na kushoto kwake ni Mkurungezi wa Uendeshaji wa
Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika hafla ya uzinduzi wa Jina jipya
la Kampuni hiyo iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa PLC Kijitonyama
Jijini Dar Es Salaam
Mjumbe
wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr. Donalth Ulomi akifanya mahojiano na
mwandishi wa habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa Jina Jipya la Kampuni ya
Maxcom Africa PLC.
Mjumbe
wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr. Donalth Ulomi akifanya mahojiano na
mwandishi wa habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa Jina Jipya la Kampuni ya
Maxcom Africa PLC.
EmoticonEmoticon