NA WAMJW DAR ES SALAAM.
WATANZANIA waaswa kujitokeza
kuchangia damu mara kwa mara ili kuondokana na tatizo la vifo
vinavyotokana na upungufu wa damu hasa kwa kina mama wajawazito nchini
wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati
alipotembelea katika tukio la uchangiaji damu lililofanyika Makao makuu
ya benki ya KCB jijini Dar es salaam.
“Marufuku kwa mtoa huduma yeyote
wa afya kuuza damu mgonjwa kwani wananchi wanachangia damu bure kwa
manufaa yao ya baadae aidha kwa wao wenyewe au ndugu zao” alisema Waziri
Ummy.
Aidha Waziri Ummy amewaagiza
Waganga Wafawidhi wa mikoa kuhakikisha wanaweka mabango yanayoonyesha
kuwa damu ni bure kwa wagonjwa wote wanaohitaji huduma hiyo bila ya
kubagua mwananchi yeyote.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema
kuwa mwananchi yeyote mwenye umri wa miaka 18, mwanamke asiye mjamzito
wala kunyonyesha na asiyekua mgonjwa kama vile kisukari,saratani na
mgonjwa wa moyo anaweza kuchangia damu.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya KCB nchini Bw. Cosmas Kimario amesema kuwa wameamua
kuaandaa uchangiaji wa damu ili kuisadia Serikali katika sekta ya Afya
hususani katika kupunguza vifo vinavyotokana na upungufu wa damu.
EmoticonEmoticon