Naibu
waziri wa Kazi,Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Ndg. Anthony Mavunde
leo amefanya mazungumzo na Balozi wa Uswisi Mh Florence Mattli katika
ofisi za Wizara ya Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu mjini Dodoma
juu ya namna bora ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi katika eneo
la Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana kupitia mpango unaotekelezwa na Wizara.
Balozi Mattli ameupongeza mpango
wa Wizara wa utekelezaji wa Program ya Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini
kupitia mafunzo stadi ambayo yana lengo la kuwajengea Vijana wa Tanzania
ujuzi stahiki na hivyo kuwawezesha kuwa na sifa za kuajiriwa,Kujiajiri
na kuajiri Vijana wengine.
Balozi Mattli ameahidi
kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono juhudi za Wizara katika
uendeshaji wa Mafunzo ya Ufundi kwa Vijana kwa kufadhili kiasi cha
Shilingi 34,000,000 USD kwa miaka 12 kwa ajili ya utekelezaji bora wa
Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini
EmoticonEmoticon