Taswira kabla ya kuanza kwa usafi wa fukwe ya Mbezi Beach ambapo ni fukwe inayotumiwa na wakazi wa Mbezi Beach na maeneo ya jirani , lakini kuna uchafu mwingi uliokusanyika pembeni hapo na kuleta kero kwa wakazi hao wanaotumia fukwe hii kwa mapumziko .
Wadau na marafiki wa bahari wakiendelea kufanya usafi katika maeneo ya fukwe hii ya Mbezi Beach ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT ,Nipe Fagio na Marafiki wa Bahari na usafi huo ulifanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita.
Baadhi ya sindano zilizopatikana wakati wa usafi wa fukwe ya Mbezi Beach uliofanyika mapema mwishoni wa wiki iliyopita ,Sindano hizi ni hatari kwa watumiaji wa fukwe hasa kwa watoto wanaocheza bila kuwa na tahadhari.
Taswira ya Fukwe ya Mbezi Beach wakati wa usafi ukiendelea
Taswira za baadhi ya takataka na chupa zilizopatikana katika fukwe ya Mbezi Beach
Mkazi wa Mbezi Beach Beatrice aliyeungana na marafiki wa bahari katika kusafisha fukwe hizo za Mbezi Beach akiendelea na usafi mwishoni wa wiki iliyopita .
Usafi ukiendelea katika fukwe ya Mbezi Beach ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT ,Nipe Fagio na Marafiki wa Bahari na usafi huo ulifanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita.
Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele ambao ni waratibu wa kampeni hii ya TANZANIA OKOA BAHARI na Afisa wa NIpe Fagio wakiwa wameshikilia moja ya sindano zilizopatikana katika fukwe hizo za Mbezi Beach katika usafi uliofanyika mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
Baadhi ya wakazi wa Mikocheni B na Mbezi Beach waliojitokeza kusafisha Fukwe ya Mbezi Beach mapema wiki iliyopita wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza usafi huo.Usafi huo ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT ,Nipe Fagio na Marafiki wa Bahari na usafi huo ulifanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita.
Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele ambao ni waratibu wa kampeni hii ya TANZANIA OKOA BAHARI akifanya mahojiano na mahojiano na mwandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kutunza fukwe na mazingira ya bahari mara baada ya kufanya usafi katika fukwe za Mbezi Beach.
EmoticonEmoticon